Rais Magufuli kuzindua rasmi Wilaya ya Kigamboni Februari 11, 2020

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho Februari 11 anatarajiwa Kuzindua Rasmi Wilaya Mpya ya Kigamboni ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa Wingi katika Uzinduzi huo

RC Makonda amesema hafla ya Uzinduzi huo inatarajiwa kuanza Saa Moja Asubuhi kwenye Viwanja vya Mkuu wa Wilaya ambapo Rais Magufuli atazindua Jengo la Utawala la Mkuu wa Wilaya, Jengo la Halmashauri na Majengo ya Hospital ya Wilaya ya Kigamboni

Uzinduzi huo unakuja wakati tayari Serikali imefanya juhudi za Maendeleo katika Wilaya hiyo kupitia Miradi mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Barabara za Lami, Ujenzi wa Hospitali, Vituo vya Afya, Zahanati, Huduma za maji, Elimu pamoja na huduma zote muhimu.
 
Back
Top Bottom