Rais Magufuli kumbe bado unawalipa uliowaita mafisadi?

Hivi hujui tofauti kati ya kufukuzwa na kusimamishwa kazi? Lazima walipwe stahiki zao maana umewatuhumu tu na hujathibitisha
Unapo msimamisha mtu kazi unatakiwa hiyo nafasi iwe wazi mpaka umalize uchunguzi !!
Sasa unapomsimamsha alafu unaleta mtu mwingine wote unawalipa mamilioni alafu unasema unabana matumizi ni upuuzi wa hali ya juu!!!
 
Naomba uniambie sheria na taratibu za utumishi wa Umma zinasemaje kwa watumishi walio simamishwa kazi?
Nyie si mnataka utawala wa sheria na taratibu? Hii ndio gharama yake! Sasa unashangaa nini mtu aliyesimamishwa kazi kuendelea kulipwa mshahara?
Mnashangaa sheria na taratibu za utumishi wa Umma kufatwa? Hapo ndio mjue kuwa Magufuli si dikteta.
 
Hoja yangu Mimi ni kumuita mtu fisadi halafu bado unamlipa elewa
 
Yes, kulipa ni lazima. Kuna nafasi zina wakurugenzi zaidi hata ya wawili na wote wanakula bingo zao kila mwezi. Kila kitu kina gharama, ukijenga mfumo na kuruhusu ufisadi kwa muda mrefu, siku ukiuchukia lazima ukugharimu pia. This is what is happening now....Kuna watu katika kundi hilo, walikuwa Manaibu Katibu Mkuu, na umri wao ni kati ya miaka 35-40. You can imagine, watastaafu lini...
 
Wewe unaezifahamu hizo sheria wanazotumia kwa wafanyakazi waliosimamishwa kazi ungemsaidia kujibu...hoja yake inakuwaje unamchafulia mtu mbele ya jamii kwa kumwita fisadi,jizi,mhujumu uchumi afu mwisho wa siku unampa stahiki zake? Huoni kuwa Rais nae anamakosa ya kuwadhalilisha wahusika ambao mahakama haijathibitisha kuwa ni mafisadi? Je serikali ikiambiwa na mahakama kuwalipa washtakiwa kwa makosa yasiyo na ukweli huoni kama wananchi walipa kodi si ndo wenye kuumia?
 
Ndo madhara ya kutokufuata sheria katika kutatua matatizo
mkuu hapo ndo SHERIA inafuatwa sasa. mtu akituhumiwa anakaa pembeni kupisha uchunguzi. na SHERIA hiyohiyo inasema lazima aendelee kupewa stahiki zake mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika na kurudishwa kazini ama kufukuzwa kazi.

asingewalipa mgesema haya;
1. raisi hafuati SHERIA. anaongoza kiimla
2. raisi haheshimu haki za binadamu, ana mtuhumu mtu na kumwachisha kazi bila malipo yeye akale wapi na wategemezi wake?

Ama kweli mwenye husda, hata kama unachezea majini atakwambia unamtimulia vumbi.
 
Kwa hiyo wakikutwa na hatia watarudisha hayo mamilioni??
 
Binafsi sijawahi kuliamini gazeti la Tanzania Daima. Huwa wanaandika kinyume
Usihofu. Kama siyo kweli kurugenzi ya ikulu itakanusha na Tanzania Daima wataomba msamaha halafu tutawafungia
 
Kwani wamefukuzwa kazi ama wamesimamishwa kazi? Kwa kawaida mtu akisimamishwa anaendelea kulipwa mshahara isipokuwa madaraka yake hayafanyi kazi

..na ni wakati gani mhusika anakuwa ametumbuliwa?

..ni wakati amesimamishwa kazi, au amefukuzwa kazi?

..wananchi wameshindwa kuielewa dhana ya kutumbua majipu. Hili ni suala la kiutaratibu na kisheria lakini sasa hivi limehamia kwenye majukwaa ya siasa.
 
Kwani wamefukuzwa kazi ama wamesimamishwa kazi? Kwa kawaida mtu akisimamishwa anaendelea kulipwa mshahara isipokuwa madaraka yake hayafanyi kazi

sasa kwanini awaite mafisadi wakati hajadhibitisha!?
 
hizo ni tuhuma tu, usipowalipa je wakishinda kesi? si tutawalipa na fidia
Kama ni tuhuma kwanini walitumbuliwa? Nini maana ya kutumbuliwa?

Je hao wengine waliowareplace si wanalipwa? Huoni hasara hiyo kuwalipa wafanyakazi wawili wenye task moja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…