kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
Kwa siku za karibuni, Raid Magufuli amekuwa akisakamwa na wapinzani na kuwa anakandamiza demokrasia.
Shutuma hizi hazikuanza Jana au juzi zilianza kitambo tangu serikali ya Magufuli ilipofikisha miezi mitatu wakaibuka wanasiasa mbali mbali kwa nyakati tofauti wakiwemo kina Mbowe na kundi lake la kina Prof Baregu.
Na hivi majuzi ameibuka mwingine General ulimwengu na wengineo wanaodai kuwa utawala wa Magufuli ni wa kidiktekta usioheshimu haki za binadamu tena Prof Baregu akafika mbali zaidi na kuufananisha na utawala wa kifashisti.
Hata hivyo sio kwamba kila lisimwalo na wapinzani na wanaharakari basi linakuwa Ni Alpha na Omega kuwa ndiyo sahihi. Binadamu ana mapungufu katika utashi wa jambo;hisia, fikra mtizamo na utoaji haki katika suala linalolenga jamii.
Ninachokusudia kusema hapa ni kwamba mwanzoni mwa utawala wa Rais Magufuli alianza na ziara za kushitukiza wapinzani na wasomi, wanaharakati na wakiwemo wapinzani ndio waliokuwa wakimpa sifa kede kede rejea Sumaye alivyomsifia Raid Magufuli alipokwenda kumuona Muhimbili kwa kushitukiza.
Sifa hizi zilianza kuwakera wadau ambao walishindwa kutambua pamoja na kusoma alama za nyakati kuwa wasingeendelea tens kuishi kwa ujanja ujanja katika mazingira ya vimemo kwenda ikulu kama awamu zilizotangulia vimemo hivyo ambavyo vilikuwa Ni maombi ya kutaka kufanyiwa mambo flank flani.
Kwa Bahati mbaya Rais Magufuli alipiga marufuku vijimemo hivyo na sio vijimemo tu Bali hata kuonana naye ikawa ni shida kubwa kabisa ambapo matokeo take mazoea hayo yakaanza kupotea taratibu na kutoweka kabisa. Hapo ndipo yalipo ibuka madai ya kuitwa diktekta na fashisti kwa Rais Magufuli yaliloanzia.
Ilifika wakati ikulu ilideuzwa kama pango la walanguzi na wajanja. Watanzania tunakumbuka huko nyuma Baba wa Taifa Mwl. Nyerere alishawahi kukemea tabia ya Ikulu kugeuzwa kuwa pango la walowezi akaishia kusema "Ikulu Ni mahari patakatifu".
Leo hii Rais Magufuli ameamua kwa dhati kusafisha jina la Ikulu ili mradi kuwa mahala patakatifu kama alivyosema Mwl. Nyerere matokeo yake wananja wachache na wapiga dili kupitia uhanaharaki ili wafadhili wao wawaone na kuwaongezea posho ndipo walipomachika jina la dikteta.
Labda watwambie udiktekta na ufashisti wa Rais Magufuli upo wapi? Au Ni hatua yake ya kukutaa ikulu kuchezewa? Au kupiga marufuku vijimemo? Nadhani hili swali la mwisho nililoliandika nadhani ndilo lnalowasumbua wakubwa na wanaharaki wetu.
Jambo lingine, tusiandikie mate wakati wino upo. Raid Magufuli anashutumiwa na kuwa amegeuka kuwa hazina ya serikali ambapo"chenji" za matumizi zinarudishwa kwake na yeye anapeleka anakotaka. Na kwamba kwa kufanya hivyo anaingilia Uhuru wa bunge.
Hoja hii Ni "mfu" kwa sababu katiba ya jamhuri ya muungano ibara ya 139(2) inampa Rais uwezo wa kuidhinisha fedha itolewe kutoka mfuko Mkuu wa serikali hazina kwa ajili ya kulipia ghaama zaa lazima za shughuli za seriali. Hivyo hajawahi kuingilia kuvunja sheria ya nchi kwa kuingilia Nazi za binge.
Kuhus tuhuma kwamba anaminya demokrasia. Ifahamike kwamba hata siku moja hajawahi kutoa tangazo la kupiga marufuku maandamano na wala pia hajawahi na wala kuagiza Spika au Naibu Spika wa bunge kuwafungia wabunge wa upinzani kutoingia bungeni.
Shutuma hizo zinakuja kwakwe kwa kuwa anawatolea nje watu mashuhuri(wakubwa) waliozoea kutuma vijimemo ili awapendelee watu wao katika masuala Fulani Fulani wanayoyajua wao. Mlango huo sasa umefungwa ndio maana siyo wapinzani tu hata viongozi wa chama chake wanamchukia kwa sababu hiyo.
Kuitwa kwake diktekta kunatokana na msimamo wake wa hapa kazi tu na kukataa maovu yaliyozoeleka siku za nyuma.
Kwa upande wangu nimshauri Rais wetu akomaye nao hivyo hivyo itafikia hatua tutakaa sawa tu hata kama hawapendi kwani dhana ya udiktekta haikuanzia kwake leo hii kwani hata wakati wa utawala wa awamu ya tatu wa mzee Mkapa aliwahi kulaumiwa hivyo na kuitwa diktekta katika kipindi chake cha mwanzo cha uongozi wake.
Shida kubwa Rais Magufuli ameonyesha kutokubaliana na matendo yasiyoendans na maadili ya uongozi. Na kwa hakika lilikuwa tegemeo la wengi kumpata Rais wa aina yake Magufuli ambaye hataki kuendekeza maovu. Kikubwa anayofanya yapo ndani ya sheria na katiba ya nchi.
Pia nimalizie kwa kuwaambia wale wote wanaohisi anaminya demokrasia wasibaki kutafuna Maneno, Bali wajitokeze hadharani wataje sheria ipi au kifungu kipi kimevunjwa na Rais Magufuli tangu aingie madarakani.