Rais Magufuli kama Florentino Perez, Usajili wa Mghwira na Mkumbo waizika rasmi ACT Wazalendo

alvinroley

Member
Sep 30, 2016
71
251
Kama ingekuwa kwenye soka Basi Rais Magufuli angekuwa ni Florentino Perez, ambaye ni Rais kichwa wa Club ya Real Madrid anayetumiaga akili sana kusajili pale Santiago Bernabeu.

Rais Magufuli kumteua Bi Mghwira kuwa RC Kilimanjaro Na Prof Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji ni Usajili Tosha wa ACT katika chama tawala. Magufuli amecheza kama Pele.

Ni nani amebaki ACT mwenye uwezo wa kupinga chama tawala? Ni Zitto? Ni Msando? Tusubiri Usajili ujao wa dirisha dogo tuone. Ila ni Rasmi sasa hakuna ACT. Na kama ipo Basi wamechomolewa mbavu za kupanda jukwaani 2020 kuipinga CCM.

Magufuli wakati fulani akiwa ziarani Unguja alisema wazi kuwa hakuna Mpinzani atakayeingia kwenye serikali yake kamwe.

Sasa hawa ACT wanaoteuliwa ndani ya Serikali tunalazmika kuamini kuwa sio wapinzani na hawakuwahi kuwa wapinzani kwa mujibu wa kauli ya Rais Magufuli.

Ushauri: Zitto kama we Bado ni Mpinzani Basi kafute Chama kwa Msajili na Na hapo utakuwa na ubavu wa kuhoji Na kukosoa CCM. La sivyo Na wewe subiri Usajili wa dirisha dogo. Chama 'Kimebakwa' sidhan kama unajua hilo.

Sasa ukiamua kubaki ACT utakuwa 'Mpongezaji' siku zote, tayari Mama Mghirwa ameshakuwa mjumbe wa kamati ya chama tawala mkoa. Maana kwenye CCM Mkuu wa mkoa ni mjumbe wa kamati ya Siasa ya CCM mkoa.

Kama ukibaki ACT na ukakosa uteuzi serikalini Basi naamini umekomolewa kisiasa. Msisahau kuwa Lipumba bado anangoja Uteuzi.

====> Rais Magufuli: Hakuna mpinzani atakayekanyaga kwenye serikali yangu

Magufuli wapinzani.png
 
Angalau ACT ina viongozi waliojipambua kuwa ni watu wenye sifa za kuongoza nchi hii.

Upande mwingine ni jalala la mavuvuzela, matusi, unafiki, hamaki, kushutumu, na kulalama ili kukidhi maslahi yao binafsi ya kisiasa - agenda yao kubwa uhuru usio na mipaka, kinyume chake ni utawala wa kidikteta.
 
CDM wako imara sana, msingi wao ni kaskazini kwa watu wenye misimamo, mapandikizo yote yanatoka kanda zingine.
Mijitu kama wewe ndio mnafanya watu wanamageuzi wengine kubwa neutral na kutopiga kura, hata Mrema 1995 alipoteza watu wengi baada ya watu wa design yako kuanza kuweka vikao vya watu wakutoka sehemu fulani tu ili Mrema awe Rais, tukastuka
 
Mijitu kama wewe ndio mnafanya watu wanamageuzi wengine kubwa neutral na kutopiga kura, hata Mrema 1995 alipoteza watu wengi baada ya watu wa design yako kuanza kuweka vikao vya watu wakutoka sehemu fulani tu ili Mrema awe Rais, tukastuka
Ukweli utabaki kuwa kweli
 
Zitto anapotezwa rasmi Kisiasa kwa kosa la kuanza Mahusiano na Mtuhumiwa Ufisadi Lowassa kujumuisha ACT kwny Ukawa kwa ajili ya 2020, Hakuna namna zaid ya Zitto kurudi Chadema au kupotea kabisa!

JPM sio Mtu wa Mchezo Mchezo
 
Back
Top Bottom