Rais Magufuli jaribu kumfikiri tena professor Muhongo, ni hazina ya taifa

Ni hazina ya taifa kwani amelifanyia taifa nini cha maana? Wewe ni muhongo mwenyewe nini? Watu wapo wengi wenye weredi kuliko huyo muhongo.
 
Nchi inasumbuliwa sana na matetemeko ya ardhi. Napendekeza kwa vile ni mtaalam wa miamba, mawe huko kuzimu, ateuliwe Waziri wa Tetemeko. Ila awe makini asirudie makosa maana Mkulu anaweza kutetemeka naye tena! Labda Bukoba wanaweza kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye maana aliwahi kwenda kuwapa pole na kujionea uharibifu wa tetemeko la Bukoba akachangisha sh 40,000 kama pole! Upo!!!
 
Hazina ipi tena. Muhongo anastahili kuishi mahabusu. Rais alisema, Bunge lilipitisha azimio la kujenga mtambo wa kuyeyushia madini na kuyatenganisha. Na muhongo amekuwepo katika wizara hiyo muda mrefu lakini aliacha nchi inaibiwa yeye anawaza namna ya kupiga. Kapiga escrow na sasa kumbe kuna baba lao dude ananufaika nalo.
Sijui alikuwa anakusanya hela ya kumsaidia kampeni kugombea uraisi au hakujua alichokuwa anakifanya. Detested with Muhongo. Yeye nawatangulizi wake hawastahili kuwepo mitaani.
Kama kuna mtu anaona Muhongo ni Hazina, pasi pendekezo liwe kumuuza tufidie sehemu ya hasara aliyolitia Taifa.
Na tunajua wapo hapa wanufaika au waathirika na utenguzi huu. Nyamazeni nyambafu.
 
Hivi hizi reports za madini huwa hazijadiliwi kwenye Baraza la mawaziri!
 
Kama ulivyoamua kutokana na mapendekezo ya kamati. Ila huyu jamaaa bado ni hazina ya taifa. Jaribu kumtumia tena kwenye baadhi ya maeneo kwenye sector ya madini.
mkuu, huyu jamaa kweli inawezekana ni mchapakazi kweli kweli.
lakini ana udhaifu mmoja - kibri, ujeuri, majivuno!
hii kupigwa chini uwaziri multiple times inawezekana ni mpango wa Mungu kumfanya ajifunze kujishusha na kunyenyekea.
mi naona hivyo!
 
Kama ulivyoamua kutokana na mapendekezo ya kamati. Ila huyu jamaaa bado ni hazina ya taifa. Jaribu kumtumia tena kwenye baadhi ya maeneo kwenye sector ya madini.
No, huyu ni mhujumu uchumi,aondoke.Hana moral authority. Nakumbuka kwa uchungu sana ile issue ya meter za mafuta bandarini, swala la kupandisha bei ya umeme na EPTL na sasa hii ya utoroshaji wa madini kupitia kwenye mchanga,huku yeye akiwa Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Nishati na Madini.He is either incompetent or a collaborator,he has to call it quits.
 
Kwa historia ya tatizo la umeme kabla hajawa waziri katika awamu ya JK na JPM, huwa namkubali sana Muhongo.
Kulikuwa na shida sana ya umeme, apipoteuliwa kuwa waziri wa nishati, tena kipindi cha mtera kunaukame tatizo likaisha kama utani. Alipoondoka akaja Simbachawene tatizo la umeme likarudi pale pale. Aliporudishwa limeisha na hatujawahi ona vichwa vya habari vya magazeti juu ya bwawa la mtera.

Sijajua alikuwa anapatia wapi kwa hili. Ngoja tuone na atakayekuja itakuwaje maana JPM alimuhitaji sana ili tupate umeme wa kutosha kuendesha viwanda.

Hili la madini sijui amejikwaa wapi, maana alijinasib ana ramani ya madini yote tanzania tena aliyoichora yeye mwenyewe.
 
Tangu amshambulie kafulila Na kumuita tumbili halafu mwishoni tumbili akaibuka mshindi!
Nilimuona muhongo ni mtu Mwenye kujivuna sana Na anataka kwa usomi wake asibishiwe anachozungumza
 
Back
Top Bottom