Rais Magufuli: Hivi mnadhani nikiondoka madarakani ndege, reli, hospitali zitajengwa? Kwanini huko nyuma hawakufanya haya?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Rais Magufuli amehoji hivi...

Je, nikiondoka leo reli itajengwa?
Je nikiondoka leo ndege zitanunuliwa?
Je nikiondoka leo vituo hivi vya Afya vitajengwa?
Mbona havikujengwa huko nyuma?Niondoke niwaache hawa watu?

Julius Kambarage Nyerere,nae hakufanya chochote?

1.Huduma za Afya bure kwa kila Raia

2.Elimu bure kuanzia msingi mpaka Chuo Kikuu,mbali na kutogharamia elimu wanafunzi walipewa Viatu,madaftari,Kalamu/Biki pamoja na Uji.

3.Vikajengwa viwanja vya michezo kila Mkoa

4.Vikajengwa Viwanda Karibu kila Mkoa (Nyuzi-Tabora,Nyama-Shinyanga,ZZK-Mbeya,Magunia-Iringa,Ngozi-Mwanza,Matairi-Arusha,Viatu-Dsm n.k.

5.Shirika la ndege likafikisha ndege 14

6.Huduma za Benki (NBC)zikatawanywa mpaka Vijijini.

7.Akajenga Vyuo vya kati na vya ufundi kila Mkoa.

8.SIDO zikajengwa kila Mkoa

9.Mashamba ya mifugo yakaanzishwa karibu kila Mkoa.

10.Wanafunzi wa Sekondari na Chuo Kikuu walilipiwa mpaka nauli za Treni ama
Mabasi na Serikali.

11.Barabara za ndani ya mikoa zilijengwa na watanzania wenyewe wakiongozwa na majeshi yetu.

12. Hotel kila mkoa

Haya ni kama asilimia 10 tu katika Yale aliyoyafanya Mwalimu Nyerere wakati akiwa Madarakani.

========

Kwa hisani ya MwanaHalisi Online:

RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kuwaombea mawaziri, akisema kwamba wanafanya kazi kwa mateso makubwa.

Rais Magufuli ametoa wito huo leo tarehe 5 Oktoba 2019, akizungumza na wananchi kwenye ziara yake mkoani Songwe.

Rais Magufuli ameeleza kuwa, katika uongozi wake mawaziri hawafaidiki kiasi kwamba watu wanawaonea huruma.

Mkuu huyo wa nchi amesema, sio kwamba hawapendi mawaziri wake bali analazimika kufanya hivyo. Na kuwa, mawaziri wake hawana uhakika na kesho yao, kama wataendelea kuwa mawaziri.
“Katika kipindi ambacho mawaziri hawakufaidika ni wakati wangu. Kwanza, hata wanapolala hajui hata kama kesho ataamka akiwa waziri. Najua watu wanawaonea huruma, lakini lazima nifanye hivyo. Sio kwamba siwapendi, wanafanya kazi kwa mateso makubwa na wao muwaombee sana,” amesema Rais Magufuli.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amesema hawezi akaondoka madarakani huku akiwaacha Watanzania hawana maendeleo.

“Unajiuliza vituo hivi (vya afya) 352 vimekamilika kujengwa, tumeokoa roho za watanzania wangapi masikini? Kweli niondoke niwaache hawa kwa sababu tu ya unafiki wangu, kwamba natakiwa niondoke nimechoka?

Hapo ndipo ninapopata nguvu ya kusema lazima niendelee kufanya kazi, na ndio maana ninawaomba sana wana Songwe na wenzangu muendelee kuniombea na kuwaambea viongozi wenzangu mawaziri wanafanya kazi sana,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema hana imani kama akiondoka madarakani, miradi anayoitekeleza, kama itafanyiwa kazi na watakaokuja baada yake.

“Lakini saa nyingine ukishajiuliza mateso ya watu ambao wanayapata, inakubidi useme lazima mimi nifanye. Ilikuwa ni lazima nifanye mimi. Ukiangalia namna ukiicha nchi, je hii miradi kweli itatekelezwa? Je, nikiondoka leo Stiglers Gorge ijtajengwa? Nikiondoka leo Standard Gauge itajengwa?” amehoji Rais Magufuli na kuongeza;

“Je, nikiondoka leo ndege zitanunuliwa? Mbona hazikununuliwa miaka yote? Hapo ndipo ninapojisikia, ninasema lazima nifanye kazi.”
 
Kipindi Cha Mkapa Pia Tulisikia Izi Story Na Kipindi Cha Kikwete Pia Zilisikika Ila Kilichotokea Wote Hamjui Kwanini Walishindwa Tena Kipindi Cha Mkapa Ilikuwa Simple Sana Ije Iwe Leo Ambapo Tupo Macho 24 Hours.

"Kama Anataka Kujua Nguvu Ya JWTZ Aje Ajichanganye Kuongeza Muda Zaidi Ya Miaka 10"

Achezee TISS na Police lakini sio jeshi hakunaga kumwangalia mtu usoni na haichukui hata dakika 30 washakuweka sehemu salama"

katika taasisi ambazo bado naziamini ni JWTZ hawawezi kuwaangusha wananchi ata siku moja.
Jeshi Letu Halina Adui Wala Rafiki Wa Kudumu"
 
"Kama Anataka Kujua Nguvu Ya JWTZ Aje Ajichanganye Kuongeza Muda Zaidi Ya Miaka 10"

Achezee TISS na Police lakini sio jeshi hakunaga kumwangalia mtu usoni na haichukui hata dakika 30 washakuweka sehemu salama"

katika taasisi ambazo bado naziamini ni JWTZ hawawezi kuwaangusha wananchi ata siku moja.
Kesho jingine au hilihili lililoingiliwa na chama cha majambazi Mkuu?

Waliomimina risasi na karma the bitch inawakodolea macho si hao unaowaongelea?
 
"Kama Anataka Kujua Nguvu Ya JWTZ Aje Ajichanganye Kuongeza Muda Zaidi Ya Miaka 10"

Achezee TISS na Police lakini sio jeshi hakunaga kumwangalia mtu usoni na haichukui hata dakika 30 washakuweka sehemu salama"

katika taasisi ambazo bado naziamini ni JWTZ hawawezi kuwaangusha wananchi ata siku moja.
ha ha si unaona anavyolifumua geshi letu na tayari amepanga safu yake hapa tujiandae tu kisaikolojia kua ngosha tupo nae sana kwa miaka mingi ijayo
 
Hata asipoondoka sawa tu! Nchi ijengwe! Tunataka maendeleo sio kupata Rais kibaraka wa mabeberu akarejesja majizi na mafisadi. JPM atawale milele! Kikwete aliulizwa na mabeberu kwanini nchi yenu masikini? Akajibu, Sijui! Hatataki marais kama hao!
 
"Kama Anataka Kujua Nguvu Ya JWTZ Aje Ajichanganye Kuongeza Muda Zaidi Ya Miaka 10"

Achezee TISS na Police lakini sio jeshi hakunaga kumwangalia mtu usoni na haichukui hata dakika 30 washakuweka sehemu salama"

katika taasisi ambazo bado naziamini ni JWTZ hawawezi kuwaangusha wananchi ata siku moja.

Hawa hawa ambao siku ya UKUTA walitangaza watafanya usafi nchi nzima?
 
Sasa ukweli unazidi kujitokeza, kufuata katiba chini ya awamu hii ya 5 ya CCM si kitu wanachokiheshimu, jambo hili linabidi lijadiliwe kwa kina. Maana tusipolijadili mapema watapeleka miswada ktk Bunge lililojaa wanaCCM kubadili katiba kukidhi wanayotamani kufanya
 
"Kama Anataka Kujua Nguvu Ya JWTZ Aje Ajichanganye Kuongeza Muda Zaidi Ya Miaka 10"

Achezee TISS na Police lakini sio jeshi hakunaga kumwangalia mtu usoni na haichukui hata dakika 30 washakuweka sehemu salama"

katika taasisi ambazo bado naziamini ni JWTZ hawawezi kuwaangusha wananchi ata siku moja.
Unaongelea jeshi hili la CDF Mabeyo, au lipi Mkuu?
 
Back
Top Bottom