magode
JF-Expert Member
- Oct 2, 2014
- 2,204
- 3,337
Wanabodi,
Salaam
Kwa hali inavyoonekana Rais wetu bado hajatofautisha kauli za kampeni na kauli km mkuu wa nchi. Wakati wa kampeni Rais magufuli alikuwa akijijenga mwenyewe bila kutumia chama chake kwa sababu ambazo kila mtu anazijua.
Nasikitika kuona kwamba Rais bado mpaka leo anatumia ubinafsi ule ule wa kampeni kujinufaisha binafsi. Km wengine wanavyolalamika,hali hiyo itampelekea kuwa dikteta.
Kwa bahati mbaya sana madikteta wote huwa wanaamini sana kile wanachofanya. Me namshauri Rais kwanza aache ubinafsi,aache kujinufaisha binafsi. Kwa sasa yeye ni Rais wa watu wote wakiwemo hao wafanyabiashara wa sukari.
Njia ya kuwakomesha hao ni kuagiza sukari kwa wingi ili waliyonayo ikose soko hadi iishiwe muda wa kutumika.
Pia haipendezi Rais kusema uongo,Rais anasema alizuia sukari eti kwakuwa iliyokuwa inaletwa ilikuwa imeisha muda wake!
Huu ni uongo wa wazi,ingawa alikuwa anashangiliwa,waliokuwa wanashangilia ni kwa sababu hawakujua km wanadanganywa. Rais alipaswa kuwa mkweli kwamba walizuia sukari nje bila kufanya utafiti. Hivi km serikali iligundua wafanyabiashara wanaingiza sukari iliyokwisha muda wake,suluhisho lilikuwa kuzuia kuingiza sukari??
Rais fanya maamuzi km kiongozi wa nchi. Hizi sifa hazikusaidii sana ww wala serikali yako wala sisi wanachi wa kawaida. Kampeni zilishaisha na wewe ndo mkuu wa nchi.
Nawasilisha..