Rais Magufuli azindua mpango wa ugawaji wa madawati kwa Majimbo mbalimbali nchini

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA MPANGO WA UGAWAJI WA MADAWATI KWA MAJIMBO MBALIMBALI NCHINI

WhatsApp-Image-20160713.jpeg

1.jpg

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimuonesha Rais Dkt. John Pombe Magufuli sehemu ya Madawati yaliyotengenezwa na fedha zilizopatikana kutokana na kubana matumizi kutoka Ofisi ya Bunge katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

5.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge wakwanza kulia Mariam Elias (darasa la tatu na wapili kutoka kushoto George Samwel mwanafunzi wa darasa la tano wakiwa wanapiga makofi kabla ya tukio la ugawaji wa madawati hayo yaliyotokana na kubana matumizi kutoka Ofisi ya Bunge.

7.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu ambaye aliyapokea kwa niaba ya Wabunge wa majimbo mbalimbali nchini.

8.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ndogo ya Tume ya huduma za Bunge inayoshughulika utengenezaji wa madawati. Waliosimama mbele ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa, Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu pamoja na Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi.
9.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya msingi Bunge mara baada ya tukio la kukabidhi madawati katika Majimbo mbalimbali nchini. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson pamoja na Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako.
10.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya Maaskari brass bendi ya Jeshi la Magereza mara baada ya kukabidhi Madawati.


12.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwanafunzi wa Darasa la tatu katika Shule ya Msingi Bunge Mariam Samwel wakati akiondoka kwenye viwanja hivyo.
13.jpg

Sehemu ya Madawati yaliyokabidhiwa leo.
14.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyehudhuria hafla hiyo ya ugawaji wa Madawati katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU.


HAPA KAZI TU!
 
Ni hatua nzuri Kwa serikali yetu Kwa kweli baada ya miaka kadhaa uhaba wa madawati itabakia history maswali ya kujiuliza je ELIMU INAYOTOLEWA SHULE ZA KATA BNI BORA AU BORA ELIMU? VIFAA VYA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA VINAKIDHI MAHITAJI NA WALIMU WANAFUNDISHA KI UZALENDO VIPI SHULE ZINAWALIMU WA KUTOSHA¿
 
Tatizo kila mtu sa hivi yuko bize na madawati na kadili wanavotumia muda mwingi ku deal na madawati watajikuta upungufu unaendelea maana hadi yataanza kuharibika, leo hii unaweza kujitolea kujenga shule/kukarabati shule ya seikali kwa zaidi ya milioni 200 ukamuomba mkuu wa mkoa aje aifungue, halafu kukakawa na sehemu nyingine mkuu wa mkoa ameitwa kupokea madawati 20 siku hiyohiyo, unakuta mkuu wa mkoa anahairisha ufunguzi wa shule anaenda kupokea madawati ili aonekane kwenye tv kumfurahisha mkuu.
Viongozi wetu wanatakiwa kuwa wabunifu na kukubali kushirikiana na wananchi kutatua kero zao, kero sio madawati pekee
 
Huu ugawaji ni wa nchi nzima (kitaifa ) ama ni few selected areas by himself? Mbona Jimbo la Iramba halipo???
 
Back
Top Bottom