Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Harakati za wabunge wa CCM kujinasua katika makucha ya TAKUKURU zimegonga mwamba baada ya Magufuli kuwabadilikia wabunge hao.
Baada ya kamata kamata ya wabunge inayofanywa na TAKUKURU na kupandishwa kizimbani Kisutu, wabunge wa CCM walipanga kuitisha kikao chao kujadili namna ya kuepukana na aibu hii, lakini Magufuli aliingilia kati na kuchimba mkwara, hali iliyopelekea kikao hicho kuyeyuka.
Mmoja wa wabunge wa CCM aliyevujisha nyeti hizi anadai mkakati ulikua pia kuwachangia wabunge wenzao ambao walikuwa wamepandishwa kizimbani tayari ili wapate mawakili wazuri, lakini hilo pia limegonga mwamba baada ya Magufuli kuwa mbogo juu ya suala hili na wakapingana wao kwa wao.
“... hali hii imefanya wabunge waishi kwa mashaka sana, kuna wakati walikuwa wanataka kuitisha kikao cha wabunge wa CCM ili kujadili hali hii lakini naona mambo yameshindikana baada ya bwana mkubwa, (Rais John Magufuli) kupata taarifa na kuwa mkali,” alisema mmoja wa wabunge wa CCM.
“Kwa kweli hii hali ya kamaka kamata siyo mzuri, inaharibu sifa yetu kama wabunge, nadhani ingetosha mamlaka za Bunge kushughulikia wale wanaotuhumiwa,” alisema Mbunge mwingine.
Mbali na wabunge, inadaiwa wakati wowote Takukuru itawafikisha mahakamani vigogo wengine wanaokabiliwa na mashitaka ya mabilioni ya Uingereza na benki ya Stanbic Tanzania.
Source: NIPASHE