Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais John Magufuli amewasili Jijini Arusha tayari kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi wanachama. Akiwa uwanjani amepokelewa na Mbunge Arumeru Mashariki ndugu Joshua Samwel Nassari wakiwemo viongozi wengine wa chama na serikali.