barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Katika Mkutano huo uliofanyika Entebbe-Uganda,ulihudhuliwa na Rais wa Kenya,Uhuru Kenyata,Rais wa Zambia Edgar Lungu,Rais wa Rwanda Paul Kagame,Waziri Mkuu wa Ethiopia na Rais wa Sudani Kusini na Mwenyeji Yowel Kaguta Museveni;Kwa upande wa Tanzania,Rais Magufuli aliwakilishwa na Balozi Augustine Mahiga.
Mkutano huo ulikuwa na lengo la kujadili juu ya Amani na usalama ktk nchi zilizohudhuria kwa msaada wa Israel,kukabiliana na ugaidi na pia kuimarisha mahusiano ya kibiashara,kijeshi na kiusalama.
Katika moja ya hotuba zake Waziri Mkuu wa Israel amenukuliwa akisema:
"Israel ni nchi ndogo, isiyo na rasilimali tangu mwanzo wake. Rasilimali pekee tuliyo nayo ni akili na mioyo yetu." Maneno ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu