Rais Magufuli ataka Bureau de Change zimulikwe, akihofia utakatishaji haramu wa fedha

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, ameitaka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) pamoja na Wizara ya Fedha kuyamulika maduka ya kubadilishia fedha maarufu kwa jina la Bureau de Change, akihofia baadhi ya maduka hayo kushiriki michezo michafu ya kuvunja sheria za nchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la Benki Kuu ya Tanzania Kanda ya Kusini – mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma, leo hii Machi 4, 2017, Rais Magufuli alisema baadhi ya maduka hayo ya fedha yamekuwa yakishiriki katika utakatishaji wa fedha haramu (money laundering) na hata biashara ya dawa za kulevya. Hata hivyo, Rais hakutoa ufafanuzi wa kina ni kwa namna gani maduka hayo yanaendesha shughuli hizo haramu.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amesema uchumi wa nchi unakuwa kwa wastani wa asilimia zaidi ya saba na kwamba, Tanzania ni miongoni mwa nchi tano ambazo uchumi wake unakua vizuri barani Afrika.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli, katika nchi hizo tano za Afrika zenye uchumi unaokua vizuri, Tanzania imeshika nafasi ya pili nyuma ya Ivory Coast. Ingawa pia hakutaja nchi nyingine alisema; “Ukiwa nafasi ya pili kutoka mwanzo,” ni jambo la kujivunia.

Mapema, Rais Magufuli alifungua kituo cha biashara cha benki ya NMB na kumtaka waziri wa fedha kuhakikisha fedha za serikali zinapitishwa kwenye benki hiyo, uamuzi ambao kwa namna fulani unalegeza masharti yake ya awali kwamba fedha za serikali ni lazima ziwekwe katika akaunti maalumu Benki Kuu na si benki binafsi, zikiwako zile zinazojiendesha kwa ubia na serikali yenyewe kama NMB.


Raia Mwema
 
Wanashiriki kwenye utakatishaji fedha na madawa ya kulevya... Kwa nini wasiwakamate kama kuna ushahidi wa hili...

Au ndio yale ya mungu wa Dar!!! Ndege wenye mbawa moja...
 
Hivi kukua uchumi kunaendana na ugumu wa maisha?! Maana kila mara tunaambiwa uchumi unakua huku maisha yanazidi kuwa magumu
 
Mwaka wa 15 sasa nasikia uchumi unakua kwa kasi unakua kwa kasi lakini hatuoni reflect yake kwa maisha yetu ya kila siku! Uchumi kukua unapimwa na wanasiasa kwa macho yao na si vigezo rasmi ya ukuaji wa uchumi! Sina hakika huyo aliesema hayo huko Ntwara alishawahi kujua GDP ya Mtanzania ilikuwa ngapi mwaka juzi jana na sasa! Yeye anaropolka tu maana ni hulka!
 
Mimi nilifikiri kampeini za uchaguzi mkuu ziliisha Oct 2015,nikiamini sasa ni kutekeleza ahadi kivitendo kumbe bado tuko kwenye kampeini lo!
 
Back
Top Bottom