dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,500
- 3,481
KAMBI Rasmi ya Upinzani imepinga tabia ya ‘kutumbua majipu’ inayofanywa na serikali ya Dk John Magufuli hivyo imewataka watumishi na watendaji wa umma waliosimamishwa au kufukuzwa kazi na mawaziri, kufungua mashauri Mahakama Kuu ya Tanzania ili kupinga kufukuzwa kwao na baadhi ya mawaziri.
Hayo yamesemwa leo katika hotuba ya maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
Kwa mujibu wa hotuba hiyo, Lissu amesema kuwa baadhi ya mawaziri waliosimamisha na au kufukuza kazi watumishi wa umma kwa jina maarufu kutumbua majipu, walifanya maamuzi hayo kinyume cha sheria.
Ameongeza kuwa Mawaziri hao hawakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo kwa sababu hawajakasimishwa mamlaka ya utekekelezaji wa majukumu yao kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 5(1) cha utekelezaji wa majukumu ya kiuwaziri.
Kutokana na hali hiyo kambi ya upinzani imewataka watumishi wote ambao wametumbuliwa wana haki na uwezo wa kwenda mahakamani na kuomba mahakama kutengua utumbuaji wa majipu uliofanywa na mawaziri wasiokuwa na mamlaka hayo kinyume cha sheria.
“Kambi rasmi ya upinzani inaamini kuwa kwenda kwa watumishi hao mahakamani hakutawasaidia pekee kupata haki zao, bali pia kutakomesha vitendo vya kuendesha nchi kienyeji na bila kufuata sheria vinavyoelekea kushamiri chini ya utawala wa Rais John Pombe Magufuli,” amesema Lissu.