Rais Magufuli amuongezea Mkuu wa Majeshi, Gen. Mwamunyange mwaka mmoja

Rais wa jamuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Pombe Magufuli, amemuongezea Mkuu wa Majeshi wa Tanzania Mwaka mmoja wa kuendelea kuliongoza jeshi la wananchi wa Tanzania

He is right make bado hajampata wa Ku replace.
 
Waliosema Pombe alipata urais bila kutarajia wapo sahihi, kilichomkwamisha ni kuwa bado hajawajua vema makamanda, ndio anawasoma. Usikute hata full names za Mwamunyange kazijua baada ya kutinga ikulu. Yeye alijua idadi ya madaraja madogo madogo na makubwa makubwa baaasi
 
Mkuu nani aliyekosa bila kutarajia na alikua amepanga kumteua nani? thibitisha kauli yako kwamba hajawajua vema makamanda.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Pombe Magufuli, amemuongezea Mkuu wa Majeshi wa Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange mwaka mmoja wa kuendelea kuliongoza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Anastahili kuongezewa .Mwamunyange kafanya kazi kubwa mno ndani na nje.Kipindi chake tumepata ushindi majeshi yetu yalikopelekwa.Chini ya uongozi wake imara mfupa uliowashinda majeshi mengi tu ya nchi nyingi wa M23 aliuweza na kuwasambaratisha.

Amelifanya jeshi kuwa la kitaalamu zaidi,kisomi na la kisasa sana.Hongera zake
 
Ilikuwa mi lazima Gen Mwamunyange ...aongezewe muda kwa kuwa Majenerali waandamizi ambao walitarajiwa kumrithi Karibu 10 wataondoka kwa mpigo ....hili no kosa la kiufundi ambalo alifanya Rais Kikwete .....kuna wakati aliwapandisha kwa mpigo wengi lakini wengi hakuangalia utumishi wao umebaki Miaaka mingapi jeshini
Umri mzuri wa mkuu wa Majeshi anapouvaa inatakiwa angalau awe na miaka 52 Ili aweze kudumu miaka 10 ....

Kuanzia cheo cha Brigadier General sidhani wangapi wana Umri below 50 ....na Kuanzia miaka 50 hadi 52 sidhani Kama kuna meja jenerali ambao wanaweza kuwa CDF ...MWAKA HUO MMOJA GEN MWAMUNYANGE ATAIWEKA SAWA SUCCESSION PLAN YA TPDF ...KWA KUANZIA TAYARI COS MPYA NA CJKT WAMEPATIKANA
 
Waliosema Pombe alipata urais bila kutarajia wapo sahihi, kilichomkwamisha ni kuwa bado hajawajua vema makamanda, ndio anawasoma. Usikute hata full names za Mwamunyange kazijua baada ya kutinga ikulu. Yeye alijua idadi ya madaraja madogo madogo na makubwa makubwa baaasi

Kwa hiyo angepita Lowasa au Membe angekuwa ameshawafahamu makamanda wote ndani ya siku tisini. ?

Tuache kashfa na kebei za kijinga, rais anaenda kwa awamu ngazi kwa ngazi wizara baada ya wizara kitengo baada ya kitengo.

Tatizo Lowasa alishaandaa serikali yake kabla hata ya kuteuliwa, na hii ilikuwa hatari zaidi kwa usalama wa nchi .
 
Anastahili kuongezewa .Mwamunyange kafanya kazi kubwa mno ndani na nje.Kipindi chake tumepata ushindi majeshi yetu yalikopelekwa.Chini ya uongozi wake imara mfupa uliowashinda majeshi mengi tu ya nchi nyingi wa M23 aliuweza na kuwasambaratisha.

Amelifanya jeshi kuwa la kitaalamu zaidi,kisomi na la kisasa sana.Hongera zake

Kwa umuhimu ndani ya TPDF ...GEN MWAMUNYANGE ndio mwenye rekodi iliyotukuka ya kimapigano baada ya Gen Musuguri .....
Musuguri alipiganisha vita vya Uganda ,na kumalizia kusafisha Vita Vya Ukombozi..mwenye operesheni maarufu ( operesheni Safisha)...
Baada ya hapo KUANZIA miaka ya 90 hadi 2005 ..Tanzania ilijihusisha zaidi na kufufua Uchumi na kukarabati vifaa na kupata vipya kutokana na pilika za vita Vya Ukombozi na kagera

gen Mwamunyange ndie naye amebahatika kuingia kwenye rekodi ya kupiganisha vita Vingi

Kama :-

Comoro
M23
( congo)
Dafur
Lebanon etc
 
Unajua tofauti ya kupiganisha Vita na Peace Keeping?

Askari anaenda Darfur miezi 18 hajawahi kufyatua hata Baruti akirudi unaenda kumpokea Airport katoka Vitani?
Tanzania imepigana vita kali zaid ni ya Sourthen of Sahara kuipigania Msumbiji dhidi ya Wareno hii vita imeizid hata vita cha Uganda.
Ukiacha Bregadia Generali Mayunga a.k.a Mto mkavu hauchimbwi dawa sijaona Askari wa Viwango vya Kimataifa labda kidogo General Twalipo.
 
Back
Top Bottom