R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,575

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imemtangza Mwenyekiti Mpya wa atakayesimamia Bodi ya bandari ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) katika kipindi cha miaka mitatu.
Akitangaza mbele ya wanahabari mapema leo Juni 15, Katibu Mkuu (Uchukuzi) wa Wizara hiyo, Dkt. Leonard Chamuriho ameeleza kuwa, kwa mujibu wa sharia namba 17 ya Mwaka 2004 ya Mamlaka ya Usimamizi wa bandari Tanzania (TPA), kifungu 6 (2) (A)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndie mwenye mamlaka ya kuteua Mwenyekiti wa Bodi, ambapo amemteua Profesa Ignas Aloys Rubaratuka kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya TPA kwa muda wa kipindi cha miaka 3.
Prof. Rubaratuka ni Mhadhiri Mwandamizi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Aidha, Waziri Mwenye dhamana ya sekta ya uchukuzi, Mh. Prof. Makame Mbarawa (MB) kwa mamlaka aliyopewa amewateua wajumbe wa bodi hiyo ya TPA kuanzia jana Juni 14.2016 kwa kipindi cha miaka mitatu (3).
Wajumbe wapya wa Bodi ya TPA:
Wajumbe hao ni pamoja na Jayne Kezir Nyimbo (Mtaalam wa Rasilimali watu na Meneja Uendeshaji, CARTECK,Tanznaia), Dkt. Francis Michael (Mhadhiri Mwandamizi Chuo kikuu cha Dar es Salaam), Bw. Azizi Massala Kilonge (Mkurugenzi Mtendaji na Mshahuri mwelekezi, AMAK Consulting).
Wengine ni Bwana Masanja Kungu Kadogosa (Kaimu Mkurugenzi Mkuu Kampuni ya Reli Tanzania-TRL), Jabiri Kuwe Bakari (Mtendaji Mkuu, Wakala wa Serikali Mtandao, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala bora), Eng. Deusdedit Conatus Vitali Kakoko (Meneja Miradi, TANROADS) na Bwana Jaffeer Salim Machano (Mkurugenzi wa Mipango na Huduma Tanzania Investment Bank).

Katibu Mkuu (Uchukuzi) Dkt. Leonard Chamuriho akitangaza wajumbe wajumbe na Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo ya TPA