Rais Magufuli amteua Mhandisi Julius Ndyamukama kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania(TAA)

Sumve 2015

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
4,415
4,060
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Richard Mayongela na kumtaka kuripoti Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupangiwa kazi nyingine

Rais amemteua aliyekuwa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania mkoa wa Dar, Mhandisi Julius Ndyamukama kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAA

Aidha, Mhandisi Ndyamukama ndiye aliyekuwa Msimamizi Mkuu wa ujenzi wa majengo namba 3(Terminal III) ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar
IMG_20190326_114106.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo Mayongela hakuwa mtu wa Aviation, hajakulia ndani ya Aviation achilia mbali kuwa na uelewa wa hapa na pale juu ya Aviation. Unapokuwa DG kwenye taasisi ya Aviation, haihitaji tu kuwa uwe umesoma bali uwe pia na ile "Aviation Culture". Huyo dogo Mayongela was too poor in such industry...ilikuwa ni siasa na propaganda nyingi. Nashukuru kwenye hili Magufuli alifanyia kazi maoni yangu niliyoyafikisha kwa njia nayojua mwenyewe.

Huyu Ndyamukama kakaa TANROADS, lakini kasimamia ile TB3 ujenzi wake, anaelewa mambo ya uhandisi ambayo ni karibu 65% ya sehemu ya sekta ya anga, suala la Management ni kama asilimia zilizobaki, nadhani ataziweza.

Hii Mamlaka nadhani ni moja kati ya Taasisi nyeti ya nchi hii ambayo kwa muda mrefu imeshundwa kuwa na watu sahihi wa kuiongoza, yaani ukifanya nao kazi, hadi unajiuliza hivi huyu naye yupo kwenye taasisi kubwa na nyeti kwa nchi kama Tanzania Airport Authority? Kwa muda mrefu imekuwa ina recruit watu wa ajabu kidogo, kuanzia uweledi wao mpaka utendaji wao.

Aviation haivamiwi, avaition inatakiwa iundwe na watu waliokulia katika "Aviation Culture"...Niliwahi kuwa na projects na shirika moja kutoka nje kuzungukia viwanja vya ndege Tanzania, mradi ambao ungekamilika, serikali ingeenda kuingia ubia na shirika hilo kuboresha viwanja.

Yaani tukawa fukitembelea Viwanja vya mikoani, unakutana na Meneja wa kiwanja wa ovyo sana sana, mpaka unajiuliza huyu alipataje hii nafasi? Na mambo mengi yalikwama na tuliusitisha mradi sababu ya aina ya watu tuliokutana nao.

Kwa hiyo, Mhandishi mpya aliyeingia afanye mabadiliko makubwa, kuanzia huo Uwanja wa JNIA mpaka huo mpya wa TB3, weka watu ambao ni well inovative.Kuna huyo nasikia bado Director sijui ndio meneja wa kiwanja JNIA, kaboronga kila wakati lakini bado wamemuacha hapo.

Alikaa hapo, kipindi Rais anakuja akakuta mashine za scanning mbovu, yeye ndio alikuwa mkurugenzi, akazunguka akarudishwa tena...hivi nchi hii haina watu innovative wa kupewa hiyo nafasi wanaendelea kuwapa hao ambao toka TAA imekuwa mamlaka 1999 wapo tu na hakuna ubunifu?

Unakuwa na kiwanja kinakosa hata CCTV? Tukio la ndege kugongwa linatokea, mnashindwa hata kuwa na CCTV footage? Halafu bado mtu anakaa ofisini kufanyaje?

Nasikia wanazindua TB3 mwezi wa tano, ili waweze kwenda mbele kuna mambo mengi sana wanatakiwa kubadili ikiwa ni pamoja ba kuleta sura mpya za watu wa Management, hasa hizi za kuongoza viwanja nk... Nashukuru hili la kufanya mabadiliko nililipigia sana kelele na mzee kalisikia manaa nilitumia njia nyingine kumfikishia ujumbe...hili nampongeza JPM.

Nitamletea tips Eng. Ndyamkama zimsaidie pa kuanzia, vinginevyo watamuangusha hapo, kuna organization culture ya hovyo sana kwenye hiyo Taasisi. Hongera JPM kwa hili.

Kwa wenzetu, kiwanja cha ndege sio tu eneo la kushuka ndege, pia ni sehemu ya taswira ya nchi inayopaswa kuwa na watu ambao ni very inovative. Sisi ni kinyume chake...na ukitaka kujua hili,basi uwe na projects na hii taasisi, kuanzia mameneja sijui ndio wakurugenzi viwanja vya mikoani mpaka watendaji.

Aviation inataka watu waliokulia kwenye sekta hiyo, unaweza kupata msomi mahali popote, lakini mjuzi wa Aviation hapatikani popote...anatengenezwa na kuwa retained. Waziri wa wizara husika amsaidie Rais katika hili...Tumeaibika kwa muda mrefu sana.

Wakati wa Prof Mbarawa nilitoa ushauri huu, aliyepo sasa anaweza kuutumia pia: Ushauri wangu kwa Waziri Prof Mbarawa juu ya changamoto na "uozo" wa Uwanja wa ndege wa JNIA
 
Back
Top Bottom