Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,712
Habari wakuu,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam katika uzinduzi wa daraja la Kigamboni.
Amemsimamisha baada ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumlaumu kwa mambo kadhaa ya kiutendaji ikiwemo kuongeza mkataba wa maegesho ya magari kwenye jiji bila kupitia mchakato wa kutangaza tenda, ulanguzi wa kodi za mapango kwenye stendi ya mabasi ya Ubungo na kusaini mikataba miwili ndani ya mwaka mmoja iliyosababisha upotevu wa mapato kwa jiji.
Pia, soma=> Dar: Wilson Kabwe anasa kwa Mkuu wa Mkoa, Makonda