My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,932
- 13,293
Hivi ni kosa la jinai kumkosoa Rais anapokuwa amekosea?
Rais ni binadamu Kama binadamu wengine wote ,huwa anakosea pia.
Akikosea ni lazima tumwambie kuwa amekosea, hatuwezi kumnyamazia hata kidogo.
Kitendo cha Rais wetu kutamka hadharani kuwa watanzania waliopo Nje ya nchi wakituhumiwa Kwa biashara ya madawa ya kulevya wanyongwe tena Haraka Sana.
Inafahamika wazi kwamba siyo kila anayetuhumiwa na Dawa za kulevya au makosa mengine ni lazima awe ametenda kweli.Kuna watu wengi hukumatwa Kwa makosa yasiyo yao.
Mwaka 2004 ktk Jimbo la Texas marekani, kuna kijani alinyongwa Kwa bahati mbaya, Cameron Todd alinyongwa akituhumiwa kuua watoto wake Kwa moto.
Mwaka 2009 ikabainika kuwa Todd hakuua na chanzo cha vifo vya watoto wake vikabainika kuwa ni nyumba kushika moto baada ya hitilafu ya umeme.
Leo hii Todd hayupo tena duniani Kwa kosa ambalo hakulifanya.
Rais anasema, wanyongwe haraka sana, anasahau kuwa kidiplomasia raia wa nchi kuuawa nje ya taifa lake ni aibu na fedheha kubwa sana. Rais anayesema tumwombee Kwa Mungu Leo hii huyu huyu anataka mauaji ya watu wake yafanyike nje ya nchi yake.
Anasahau kuwa wakati wa kampeni alisema hautatuangusha leo tena anataka tuuawe.
Kuna watu wanabebeshwa mizigo ya madawa bila kujua, si wote ni wauzaji wa kudhamiria.
Mwaka juzi wakati wale Wa Australia wakinyongwa Indonesia, rais wa kipindi Wa Philippines alimwombea asemehe raia wake aliyekuwa kabebeshwa mzigo wa madawa bila kujua.
Hii ni aibu Sana Kwa rais kupania mauaji ya watu wake.
Sawa tuendelee kumwombea.