mzalendo iq1
JF-Expert Member
- Mar 10, 2020
- 1,257
- 1,543
Habari wadau,
Poleni na majukumu ya kazi leo. Napenda niwape pole wapinzani wote wa Magufuli hasa Ufipa guys walioko humu JamiForums.
Magufuli amezidi kushinda kila mtego na matarajio ya vibaraka wachumia tumbo na wapinzani wake wote. Baada ya janga la Corona kuzikumba nchi za mabara ya nje watu walikuwa bize kumponda Magufuli kisa tu kumtaka afunge mipaka yake wakaiga kelele ambazo zilitaka kidogo kuleta matunda kwa upande wao, sababu raia waliingiwa na uoga na kuanza kupaniki lakini Maguful akasimamia misimamo yake. Ambayo mpaka sasa bado ina faida kubwa kuliko hasara. Wapinzan walienda mbali zaid kwa kusema nchi hii inaangamizwa na uongozi wake, yaani wakimaanisha serikali.
Kwanza nimpongeze magufuli kwa kufata njia zake za kupambana na Corona. Sio kufata watu wa mabara ya nje wamesema nini. Nchi kama Tanzania huwezi kuwafungia watu wasitoke na ukaona ndio sababu ya kupambana na janga la Corona, sio kwel kwa nchi zetu njia hio ni ya kuongeza majanga kama njaa, uhalifu na korona yenyewe. Leo Uganda raia wameanza kupigwa risasI kisa tu wametoka nje. huu ni ujinga mkubwa wanaufanya watu wote wa mataifa yalio fungia watu ndan nawaambien mkitaka kuamin kuwa watu hawajamaliza tatizo bali wamejiongezea matatizo, tuanze kuhesabu siku tano kuanzia sasa katika nch zote za Africa zilizofunga watu wasitoke nje, majibu mtayapata tu.
Leo Kenya imetengua kauli baada ya mambo kuwa magumu kwamba watu wanatakiwa kutoka nje kuanzia saa 11asubui mpaka 11jion na ndio wamefunga watu siku nne tu, vipi ukiwapa wiki?
Wapinzani walitaka Maguful afunge mipaka pia atangaze lockdown nchi mzima sababu walijua maisha yatakua magumu na itakua rahisi kwao kuwashawishi watu kufanya uhalifu na kutengeneza makundi sababu hata al Shabab iliyotokana na njaa Somalia, wala sio jihad. Kama mnakumbuka kipind Somalia kuna njaa kali ndio kipindi kilichotumika kuwatengeneza al Shabab hio. Sio Tanzania tu hata nchi zingine kama janga litaendelea kuwa hivi, nchi nyingi utawala wa Sheria utavunjika sababu watu wataamua kutumia nguvu ili tu wale, yaani mwenye nguvu kuchukua kwa nguvu kitu kwa mnyonge.
Kwanini nampongeza Magufuli
Nampongeza kwa sababu ya hatua alizo chukua leo raia wa nchi zote za jirani wanatamani Marais wao wajaribu kuiga kwa Magufuli. Kuziba mipaka na kuweka watu lockdown siyo suluhu; suluhu ni dawa ipatikane, huwezi waambia watu wasitoke nje wakae ndani tu kwa tatizo ambalo hujui linaisha lini. Mkiweka watu lockdown na ugonjwa ukakaa miezi mitano mbele, tena watu mtawalisha nini na pia usalama hautakuwepo hata kidogo. Watu watakufa kwa njaa na kuuliwa kushinda hata watu watakaokufa kwa Corona.
Ningependa nimshauri Magufuli alivyokataa njia zao za kutaka kutudhoofisha sababu wanajua kabisa wenyewe wakiwa kwenye majanga alafu Waafrika wakaendelea na mambo yao, huenda likawa tatizo kwao baadaye. So wanaona watujaze ujinga kwa kujifungia ndani wakati bajeti ya mtu wa kawaida Tanzania alionayo ndani huenda isizidi hata elfu 20. Sasa hio mtu atakaa ndani bila kufanya shughuli yoyote kwa muda gani? Huku si kutaka kushikana uchawi? Wanasema usitake kutatua matatizo yako kama tajiri anavyoyatatua ilihali wewe ni maskini, buni mbinu zako.
Hapa ssa serikali yetu hatutakiwi ikae kijinga. Madokta tunao, vifaa tunavyo, mitishamba tunayo. Tusikae tunasubiri Wazungu wagundue dawa. Tunatakiwa tufanye na sisi hata kama tutafeli, but tumejaribu pia. Huwezi jua Mungu katupangia nini.
Mh. Magufuli, ama utasikia please anzisha team ya utafiti watu watafute dawa kwani suluhu sio kufunga watu wasitembee, suluhu ni kupata dawa. India raia wameshachoka kufungiwa ndani na kuchapwa fimbo sasa hivi ni askari ndio wanaochapwa. Kiufupi Tanzania tumeonyesha tuko tofauti na propaganda zao. We're fighting kwa njia zetu wenyewe. Ni kwel wanasema jaribu kufata ushauri but unaangalia huo ushauri kama unafaa.
Kusema kweli kuna watu Tanzania walivyo na roho mbaya wanatamani Corona iripuke puu ianze kuua watu wengi ili mradi tu wapate kitu cha kumlaum Magufuli sababu wao Magufuli akipata credit, kwao ni hasara kubwa. Yaani mambo yao yanakua hayaendi. Kama muda huu wameamua kukomaa na kwamba serikali inaficha idadi sahihi ya wagonjwa, basi mtuambie majirani zenu wanaoumwa serikali inawaficha?
Rais Magufuli kwa hili kapatia acha watu waendelee kufanya mambo yao Ila mipaka iendelee kuangaliwa kwa umakini ndugu zetu wa East Africa hali imeshakuwa mbaya; unaambiwa siku si nyingi vurugu zitaanza baina ya serikali na wananchi, kitu ambacho apa hakiwezi kutokea, na waliokuwa wanaombea tayari wameshafeli.
Pia, China mkumbuke sio kwamba Corona imeisha, ila wanawaza wataishi vipi bila kufanya kazi. Marekan yenyewe imeamua kufanya mipango ya kuwaruhusu watu kurudi kwenye majukumu yao kabla ya Pasaka. Hakuna nchi yoyote hapa inaweza kupambana na Corona kwa kufungia watu ndani, labda wakubali kufa njaa.
Na kingine nahisi labda huu ndio ule mda Magufuli aliosema kuwa watakuja kutuomba msaada. Mungu asaidie tu Corona iendelee kua hafifu hivihivi Tanzania, tena ikiwezekana tuanze sisi kupata dawa. Inshallah, Mungu atabariki.
Wazee wa Ufipa karibuni kuanza kutukana. Ngoja nianzee mimi kuwatolea baadhi ya point zenu:
Rudi shule hujui kuandika, kachukue buku saba yako, na mengine mengi. Ila Magufuli genious kwani mpaka hapa yeye mshindi.
Narudia tena, kuna watu walimwita Magufuli mzembe lakini wao walijua kabisa wana wagonjwa majumbani kwao ila wakazunguka baadhi ya mikoa na kuita waandishi wa habari na kufanya press conference, baadae ndio wanakuja kusema wanakaa karantini. Sijui nia yao ni nini hasa.
Sent using Jamii Forums mobile app