manywangari jean malonkwa
Senior Member
- Mar 17, 2016
- 193
- 188
Moja ya nukuu maarufu ya Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni kuwa katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977 ilikuwa inampa madaraka makubwa sana( alienda mbali kwa kusema ingemuwezesha kuwa dikiteta kama angeamua).
Rais Magufuli baada ya kuchaguliwa, Nchi ya kwanza kuitembelea ni Rwanda, Nchi ambayo Rais wake naye ana nguvu sana labda kama zile alizowahi kuzizungumzia Kambarage Nyerere. Bwana Kagame pamoja na mapungufu yake mengi lkn ni ukweli usiopingika ameifanyia makubwa Rwanda, wote tunajua baada ya yaliyotokea miaka 22 iliyopita Rwanda imepiga hatua kubwa mno kimaendeleo japo kidemocrasia na utawala bora kuna changamoto nyingi, lkn ukweli uko pale pale.
wanyarwanda wamepiga hatua kimaendeleo hasa kiuchumi. Lkn si Rwanda tu Nchi kama Russia, China na nyingine nyingi za Mashariki ya kati na mbali ambazo zimepiga hatua kubwa kimaendeleo utagundua kwenye upande wa democrasia na utawala bora hazifanyi vizuri. Ukiangalia ni kama kuna ugumu wa Nchi zinazoendelea kupiga hatua kiuchumi na kidemocrasia kwa wkt mmoja, labda kutokana na aina ya wanasiasa wa Nchi hizi ambao hawaaminiki hasa linapokuja swala la masilahi ya taifa na mikono ya wakubwa ambao wakati mwingine hutumia democrasia hasa uchaguzi kuzivuruga Nchi zinazoendelea.Hivyo baadhi ya viongoz wameamua kuchagua kimoja hasa swala la uchumi huku democrasia na utawala bora likipigwa chini.
Tanzania ni moja ya Nchi ambazo wanasiasa wamekuwa wakitumia muda mwingi kufanya fujo na michezo ya kisiasa badala ya maendeleo, tumeshuhudia miaka kumi iliyopita tukitumia muda mwingi kufanya malumbano ya kisiasa kuliko kupiga hatua za kimaendeleo, pamoja na kuonekana siasa zikikuwa na wanasiasa kibao wakiibuka lkn watanzania ambao kimsingi wanatakiwa wanufaike na siasa hzo wamezidi kuwa masikini wa kutupwa.
Labda ni kutokana na siasa hizi za Fujo na matukio ambazo kiukweli zinaonekana kutowanufaisha watanzania Bali wanasiasa huku wakipokea mamilioni ya fedha kila mwezi, Magufuli sasa ameona aitumie kikamilifu katiba ya 1977 ambayo kimsingi inampa mamlaka makubwa akiamini anaweza kuyatumia mamlaka hayo kufanya kile ambacho Kagame, Putin, mtangulizi wa Xiping, Xiping wengine kutengeneza uchumi wa taifa hiki ambao limeshapoteza mda wa kutosha ikifanya siasa huku ikipata maendeleo kiduchu.