Rais Magufuli akutana na Jaji Warioba, Benjamin Mkapa Ikulu Dar es salaam

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Januari, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu Jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Mkapa amesema lengo la kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na watanzania kuiongoza nchi, kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka Mpya.

Rais Mstaafu Mkapa pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya hivyo.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba pamoja na kumtakia heri ya Mwaka Mpya, amempongeza Rais Magufuli kwa jinsi alivyoanza kazi vizuri hususani katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo yanawahusu wananchi yakiwemo afya na maji.

Jaji Warioba ameongeza kuwa Watanzania wote wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi kubwa anazofanya, ambazo ni kukomesha rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa mali ya umma.

"Lazima kila mmoja amuunge mkono Rais, tusije tukamuachie, pale ulipo kama ni mambo ya rushwa uanzie hapo hapo, kama ni mambo ya matumizi mabaya ya madaraka anzia hapohapo, tusije tukamuachia Rais pekee yake, yeye awe kiongozi wetu, lakini watanzania wote tushughulike na matatizo hayo" alisisitiza Jaji Warioba.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

07 Januari, 2016
8dgxgxg.JPG

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam alipomtembelea January 7,2016.
3ggggb.JPG

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamini William Mkapa, Ikulu jijini Dar es Salaam alipomtembelea January 7,2016.
 
Haya tusikie nao wameenda kuomba nini sijui.
Mzee wangu Mkapa is driven by guilt conscious, sasa anataka kujisafisha kupitia mgongo wa Magufuli.
Angekuwa ni mtu wa kusikiliza ushauri na kuacha tamaa zake za mali i'm sure he could have been the best president ever!!!

Nimesoma kitabu na baadhi ya hotuba zake, mzee anajutia. Sema huwa si mtu wa kukubali makosa moja kwa moja.
 
Last edited by a moderator:
Ase-wacha tuendelee kusubiri hizi sinema! Hakuna movie iliyokosa kuwa sterling! Taratibu naona hawa wazee kwa mafungu wanamekwenda Ikulu kujibu baadhi ya maswali ya MMM kwa kunong'onezana na Magufuli!

CC Mzee Mwanakijiji
 
Hawamshauri lolote ila wanamkumbusha kuwa yeye ni ccm na jitihada zao zimemfanya awe hapo.

Labda Warioba kama anamkumbusha Maoni ya Wananchi yaliyochakachuliwa na 6.
 
Go JPM Go.

Tumia hekima na Busara zao hao wazee, but we'l support you JPM
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Januari, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu Jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Mkapa amesema lengo la kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na watanzania kuiongoza nchi, kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka Mpya.

Rais Mstaafu Mkapa pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya hivyo.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba pamoja na kumtakia heri ya Mwaka Mpya, amempongeza Rais Magufuli kwa jinsi alivyoanza kazi vizuri hususani katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo yanawahusu wananchi yakiwemo afya na maji.

Jaji Warioba ameongeza kuwa Watanzania wote wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi kubwa anazofanya, ambazo ni kukomesha rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa mali ya umma.

"Lazima kila mmoja amuunge mkono Rais, tusije tukamuachie, pale ulipo kama ni mambo ya rushwa uanzie hapo hapo, kama ni mambo ya matumizi mabaya ya madaraka anzia hapohapo, tusije tukamuachia Rais pekee yake, yeye awe kiongozi wetu, lakini watanzania wote tushughulike na matatizo hayo" alisisitiza Jaji Warioba.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

07 Januari, 2016
View attachment 315397
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam alipomtembelea January 7,2016.
View attachment 315398
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamini William Mkapa, Ikulu jijini Dar es Salaam alipomtembelea January 7,2016.
Anasema lazima kila mtu amuunge mkono???huyu mzee amelewa sifa maana hana uwezo kisheria kumlazimisha mtanzania kumuunga mkono mtawala
 
Ase-wacha tuendelee kusubiri hizi sinema! Hakuna movie iliyokosa kuwa sterling! Taratibu naona hawa wazee kwa mafungu wanamekwenda Ikulu kujibu baadhi ya maswali ya MMM kwa kunong'onezana na Magufuli!

CC Mzee Mwanakijiji
Wanaenda kusisitiza kuwa chama ndio kinashika hatamu
 
Mkapa angeacha tu ki..here..here..mbona wenzake wamejipumzikia yeye kinacho muahangaisha ni nini?
 
Haya tusikie nao wameenda kuomba nini sijui.
Mzee wangu Mkapa is driven by guilt conscious, sasa anataka kujisafisha kupitia mgongo wa Magufuli.
Angekuwa ni mtu wa kusikiliza ushauri na kuacha tamaa zake za mali i'm sure he could have been the best president ever!!!

Nimesoma kitabu na baadhi ya hotuba zake, mzee anajutia. Sema huwa si mtu wa kukubali makosa moja kwa moja.
Hivi ile tuzo ya mshikaji wa sudan ilimkosaje mkapa?au labda atapewa mkwere
 
Hao wastaafu naamini wamempa ushauri wa kujenga, sio yule mstaafu alieenda peke yake jana. ...simwamini.
 
Back
Top Bottom