sonofobia
JF-Expert Member
- Jun 21, 2015
- 947
- 3,651
Mimi binafsi napendezwa na hatua mbalimbali anazochukua rais wetu John Magufuli... Lakini lazima atambue kama kweli amedhamiria kufanya reform hizo reform zitawagusa watu wengi ndani ya chama na nje ya chama yani makundi yote wa juu na wa chini.. Kelele nyingi tumeanza kuzisikia toka kwa makundi mbali mbali
Kuna kundi la ukawa ili lenyewe linafanya siasa kwa kuwa ndio kazi yao wapo sahihi kabisa maana bila kufanya hivyo mkono hauendi kinywani.
Kuna wana Ccm wanaoamini kwenye mfumo awa ni ccm damu, awa wanaona kama umekuja kuvuruga utaratibu uliozoeleka awa ndio wanaweza kupambana na wewe mpaka dakika ya mwisho ila mpaka sasa umewavuruga.. Kwa kutumia busara wanakupinga kwa kukaa kimya hawatasema lolote ila hawakubaliani na wewe.
Kuna wafuasi wa JK awa wanaona unamuaibisha kipenzi chao, wanaona hauapreciate zuri lolote la Jk awa sasa hivi wameanza kuzungumza lugha moja na ukawa na soon watatoka hadharani kukupinga wazi wazi.. Time will tell
Kuna wananchi wa kawaida awa wapo aina nyingi wapo wanaokuona maamuzi yako yamekosa ustaarabu japo mengi ni mazuri, wapo waliotarajia matokeo kwa muda mfupi ila mpaka sasa wanaona unawacheleshea wanachotarajia
Kuna waliokuwa wananufaika na mfumo uliopita ambao almost kila mwananchi bila kujijua alikuwa ni jipu. Ila kuna wale mapapa kama wafanyabiashara wakubwa, wahisani nk ambao umefanya biashara zao kuwa ngumu awa ndio hatari zaidi maana bado awaamini kama ni kweli mambo yamebadilika wapo tayari kutumia pesa zao kukuhujumu ili kulinda maslahi yao.
Nachoshauri :
Rais apunguze kuongea kwenye public maana ameonyesha ana udhaifu wa kuweka akiba ya maneno.. Awe anaonekana kwenye media kwa nadra na akubali kuwa sio kila anapoalikwa basi aende anaweza kutuma mwakilishi au akaenda bila kuongea.. Kuonekana sana kunamfanya achokwe mapema na hotuba zake pia zimezidi ukali sehemu nyingine ni za kwenda kutangaza mazuri sio kila wakati ni ubaya pekee.
Kingine rais wetu ni mtu wa bara watu wa bara sio wazuri sana kwenye utani.. Kuna utani anafanya ila namna anavyotania watu wanachukulia serious mfano kupiga mbizi, kuchomoa matairi, vilaza nk
Kingine nachokiona ni rais kuidharau siasa na kuwa mwana mapinduzi lakini atambue siasa ndio inaendesha kila kitu na awezi kufanikiwa bila kufanya siasa so hasiache kufanya maamuzi ya kisiasa.. Akiiacha siasa kuna watu watatumia siasa kummaliza ndani na nje ya chama chake...
Mwisho kabisa awe na subira awezi kufanya kila kitu kwa wakati mmoja najua amekuwa over ambitious ila vitu vingine avipeleke taratibu maana wanadamu hawana jema ata Jesus aliishia kuuwawa na wanadamu, so afanye vitu kwa hatua muda bado anao asiogope maneno hayo yapo tu ref ishu ya sukari alikosa subira.
NB asiwaamini sana washauri wake.. Sio wote wanamtakia mema
Ni hayo tu!