SANCTUS ANACLETUS
JF-Expert Member
- Mar 5, 2016
- 3,338
- 4,675
Ulituomba tukuamini wewe hata kama hatukuiamini tena CCM.Ulitusihi tukuamini na usingetuangusha kama vile CCM ilivyokuwa imetuangusha.
Tulikuelewa na tumekuamini sana.Tunaelekea kukuamini upeo.Tunaomba nawe utuamini.Ni zamu yako nawe kutusikiliza.Maisha ni kutoa na kisha kupokea.Tulitoa masikio na mioyo yetu.Ni wakati wako nawe kutoa.Miongoni mwa tunayokuomba kutoa ni kutoendelea kubebeka katika mbeleko ya CCM.Utatuletea tena matatizo makubwa baada ya kuondoka.
Hivi umemuelewa vizuri jana Mzee Butiku juu ya alichokueleza? Ni hivi CCM iliyopewa uweza wa kufanya kazi kama Jua ilishaishiwa nuru na nguvu ya kuangaza nchi yetu.CCM yenye wasomi waliokabidhiwa dhima ya kutoa dira walishakuwa Mbwa vibogoyo.CCM ilishakuwa Tarumbeta lisilotoa sauti zilizopangilika.CCM ilishakuwa Gitaa linalotoa midundiko ambayo wachezaji(wananchi) badala ya kucheza wamevaa nguo wachezaji wakicheza wanavua nguo.Ndio watanzania wakicheza midundiko inayocharazwa na CCM wanasanua nguo zote na kuzitundika kichwani na kisha kuanza kukimbia hovyo hovyo.Matokeo yake ndo hayo mambo yanayokuliza mtu mzima.Watu wanauza nchi.Unalilia peke yako.Unanibisha? Nionyeshe machozi ya Kinana.Nionyeshe machozi ya Bulembo. Nionyeshe machozi ya Ndugai hapo jana.Ndugai jana maneno yake yalikuwa ya muombolezaji tu na si ya mfiwa! Upo hapo?
CCM,Mzee Butiku amesema sio majasiri kitambo! Kwa nini unaendelea kung'ang'ana na CCM? Kwa nini unataka tukikuamini basi tuiamini na CCM wakati huo huo? Sisi tumekuamini wewe peke yako.Kwa nini unalazimisha tuiamini na CCM pia?
Hivi una maana gani kumpa Ndugai kazi ya kuangazia uchunguzi mikataba iliyosalia ya Rasilimali zetu zingine za Asili kama Gesi, Almasi na Mafuta? Hivi Ndugai amezaliwa Leo? Hivi unafikiria Ndugai anao uwezo wa Kijasiri na wa Kiakili wa kutokuwa "compromised" na wezi kama wale waliojaribu kuwa-compromise wateule wa Kamati zako?
Hivi Ndugai angekuwa msomi jasiri alishindwaje kutengeneza "miundombinu" ili Chenge asiwe Mwenyekiti wa Bunge? Ndugai angekuwa Msomi Jasiri alishindwa nini kumpiga "Kafumu" "Magongo" ya Kimkakati ili asiweze kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini?Hivi aliwezaje kumpiga mwenzie magongo kichwani hadi akashindwa kuwa Mbunge na akashindwa kwa hao niliowatolea mifano na wengineo?
Hivi Wabunge wa CCM wangekuwa Wasomi Jasiri kama wewe kama alivyokuchora Mzee Butiku walishindwa nini kuyaona mambo haya ya kuibiwa watanzania na kufanywa mazuzu kwa rasilimali zetu?
Orodha ya mambo yanayowafanya CCM wasiwe na sifa ya Ujasiri ni ndefu sana.Itoshe wewe kuona kuwa nje ya wewe CCM hawatufai.Achana nao.Acha kuendelea kubebeka nao.CCM ni fisi.Wako wanaongozana na wewe wakinyatia "mnofu" ulioubeba(rasilimali zetu).Nakuambia ukiutua tu wanao.Ukiondoka madarakani watatushambulia haijapata kutokea!
Ndiposa tunakuomba utuamini.Achana na CCM kabisa.Anza kuasisi "Jua" lingine la kuangazia nchi yetu iwapo utang'ang'ania kuondoka 2025.Tengeneza Chama kingine chenye watu jasiri.Tuachie Chama kisichotuchezesha Makhirikhiri na hivi watanzania kuvalia nguo zetu vichwani.Acha Kabisa.