Rais wangu Magufuli nakusihi uache kuwaumiza wafanyakazi. Acha kuwatesa watanzania. Wewe ni mtesaji. Malengo na nia yako haifahamiki.
Haiwezekani kuwanyanganya wafanyakazi kile kidogo ambacho walikuwa nacho.
Umeingia madarakani ukawakuta watu wapo na madaraja yao mapya na wengine walishaanza kutumbukiziwa fedha wewe ukaIchukua. Huu ni ushetani.
Watu walishaingia makubaliano na bodi ya mkopo kulipa asilimia 8 wewe na serikali yako ukapandisha mpaka kufika asilimia 15 huo ni ushetani.
Watu wanadai madai yao. Ni madai ya malimbilizo ya Mishahara baada ya kupandishwa muda mrefu wewe ukayachukua na kuyapoteza. Huu ni ushetani.
Watu wanadai nauli zao. Wewe ukazipotezea.
Vijana wanahangaika. Tangia uingie madarakani hakuna ajira. Je huko ni kuinyosha nchi au ushetani?
Maisha yamekuwa magumu wewe umasema unainyosha nchi. Kwa nini usiseme unaipindisha nchi?
Umeleta ukaguzi wa vyeti wa kisanii. Watu wamepoteza ajira. Tena wengine walikuwa wamebakiza muda mfupi kustaafu. Kinachoshangaza ilipobainika kuwa Makonda hana cheti hujamtumbua. Sikuelewi. Tena nilikushangaa sana kukuona na wewe Unacheza wimbo wa wale wanakwaya wa Mwanza unaowataka viongozi watende haki.
Mbona nchi haieleweki inakoelekea. Mtu akiwa mpinzani kwako ni shetani.
Ukiambiwa ukweli wewe Unatisha kwa maneno kibao. Mara mimi sijaribiwi( Tambua asiyejaribiwa ni Mungu pekee). Mara mm mtu akiningilia ndiyo amepotea kabisa. (Anayeweza kumpoteza mtu ni Mungu pekee). Hata ukimshusha mtu Mungu atampandisha kwa wakati wake. Anyway sisi tunasubiri wakati wa Mungu. Mungu atatenda.
Nakusihi Rais mwogope Mungu. Tambua upo hapo kwa kibali cha Mungu.