Rais Magufuli aamuru Madaktari walioomba kufanya kazi Kenya waajiriwe nchini mara moja

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Rais John Pombe Magufuli ameamuru madaktari 258 waliokuwa wameomba kufanya kazi Kenya waajiriwe mara moja nchini Taarifa na Mh, Ummy Mwalimu Waziri wa Afya.


=====
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO​



TAARIFA KWA UMMA


AJIRA YA MADAKTARI WA TANZANIA NCHINI KENYA​

Mnamo tarehe 18 Machi 2017 Ujumbe wa Serikali ya Kenya ukiongozwa na Waziri wa Afya Dkt. Cleopa Mailu uliwasili nchini ambapo ulikutana na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madhumuni ya kuomba kuajiri kwa Mkataba Madaktari wa Tanzania mia tano (500) ili kupunguza uhaba wa Madaktari nchini Kenya. Mheshimiwa Rais alikubali ombi hilo.

Tarehe 18 Machi, 2017 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilitangaza nafasi hizo za ajira kwa Madaktari wa Tanzania kwenda kufanya kazi nchini Kenya. Maombi hayo yalipokelewa ambapo hadi tarehe 27 Machi, 2017 ambapo jumla ya maombi takribani 496 yaliwasilishwa.

Baada ya kufanya uchambuzi wa maombi haya ilibainika kuwa, Madaktari 258 walikidhi vigezo vilivyotakiwa kwenda kufanya kazi nchini Kenya. Baadhi ya vigezo hivyo ni pamoja na:

Uhakiki wa vyeti vya taaluma na vyeti vya Sekondari.

Chuo alichosoma na mwaka wa kuhitimu masomo.

Sehemu alikofanya mafunzo ya vitendo (Intership) na mwaka wa kuhitimu mafunzo hayo.

Uzoefu wa kazi.

Umri wa mwombaji usizidi miaka 55.

Usajili wa mwombaji katika Baraza la Madaktari la Tanganyika.

Asiwe mtumishi wa Umma, Hospitali Teule za Halmashauri na Hospitali za Mashirika ya hiyari wanaolipwa mishahara na Serikali.

Wakati Serikali ya Tanzania ikiendelea kukamilisha utaratibu wa ajira za Madaktari wake nchini Kenya ikiwa ni pamoja na kutangaza nafasi hizo za kazi na kufanya uchambuzi wa maombi ya kazi, kuandaa Hati ya Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Kenya kuhusu ajira hizo za Madaktari na Mkataba wa Ajira kwa Madaktari hao, wananchi (Madaktari) watano wa Kenya waliwasilisha pingamizi Mahakamani kuitaka Serikali ya nchi yao kusitisha kuajiri Madaktari kutoka Tanzania.

Kwa kuwa ratiba ya utekelezaji wa ajira hizi za Madaktari ilikubalika na pande zote mbili kuwa iwe imekamilika ifikapo tarehe 6 Aprili, 2017 na kuwa Madaktari hao wawe tayari kusafiri kwenda nchini Kenya kati ya tarehe 6-10 Aprili, 2017 na kwa kuwa hadi tarehe ya taarifa hii Mahakama nchini Kenya haijaondoa pingamizi lililofunguliwa kuhusu ajira za Madaktari wa Tanzania nchini Kenya.

Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameamua kuwa, Madaktari hao 258 ambao waliokuwa tayari kwenda kufanya kazi nchini Kenya waajiriwe na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara moja.

Kufuatia uamuzi huu, Majina ya Madaktari husika na vituo watakavyopangiwa kazi yatatangazwa katika tovuti ya Wizara www.ehealth.go.tz pamoja na wataalamu wengine wa Afya 11 walioleta maombi yao na kukidhi vigezo.

Aidha, Serikali ya Tanzania itakuwa tayari kushughulikia upya ombi la Serikali ya Kenya kupatiwa Madaktari 500, pale ambapo hakutakuwa na vikwazo vya kupeleka Madaktari wetu nchini Kenya.

Imetolewa na:

Ummy A. Mwalimu (Mb),
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto,
Chuo Kikuu cha DODOMA,
S.L.P. 743,
DODOMA.

19 Aprili, 2017
 
Rais John Pombe Magufuli ameamuru madaktari 258 waliokuwa wameomba kufanya kazi Kenya waajiriwe mara moja nchini Taarifa na Mh, Ummy Mwalimu Waziri wa Afya.

Taarifa zaidi zitakujia hapa hapa.....
Mtu mmoja mwenye shamba alipata bahati akachimba chimba chimba akakuta alumasii loloo bahaatii loloo bahaatii loloo bahaati ya mwenye shamba ×2 huu wimbo umenikumbusha mbali sana kweli ya kale dhahabu
 
Jama!!..Hii ya kuajiri madaktiari bajeti yake ilipita lini Bungeni??..Na ni kwanini haikutekelezwa muda muafaka hadi leo ipigiwe chapuo?...
Hapa naanza kuona tatizo likiwa wazi na tukiendelea nalo Tanzania itaishia shimoni!..Kila jambo hupitishwa bajeti bungeni! Hatukurupuki tu!
 
Kwani kama ajira zipo kwanini asitoe watu waajiriwe?

Hii nchi ni yetu sote, kuna watu wengine wanadhani ni yao peke yao

Sasa kati ya hao 258 na wale ambao hawakuomba kwenda Kenya nani mzalendo?
Hao 258 wana utayari

Kama wameweza kujitoa kwenda Kenya basi wapo competent na ni watu wa kazi

Jpm kwahili nampa pongezi .

Somo hili
 
Hii ni mbinu pia mujarabu ya kupata watu wenye vigezo vinavyotakiwa,maana najua vilaza hawakuomba hapo na Rais alishasema haajiri vilaza."Woga wako ni umasikini wako"wapo waliokuwa na vigezo lakini walipuuza na kubeza sasa imekula kwao.
 
Back
Top Bottom