Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,941
- 19,130
Rais amesema chuo hakifanyi biashara kwa hiyo kukitoza kodi ya bilioni 2 ya ardhi, itakuwa sivyo, pia amesema hati ya umiliki wa ardhi Dodoma yapaswa kuwa miaka 99 kamailivyo mikoa mingine na sio miaka 33.
Rais John Magufuli ametoa maagizo kwa uongozi wa Mkoa wa Dodoma (Makao Makuu ya nchi) kubadilisha hati ya umiliki wa ardhi katika mkoa huo kutoka miaka 33 hadi miaka 99.
Kabla ya kuondoka mkoani Dodoma, Rais Dkt Magufuli alifanya kikao kifupi na viongozi wa mkoa huo na kutoa maagizo juu ya umiliki ardhi mkoani humo.
Rais Magufuli alisema kuwa hati za umiliki wa ardhi mkoani humo zibadilishwe na kuwa miaka 99 badala ya miaka 33 iliyopo sasa. Alifafanua kwamba, haiwezekani maeneo mengine ya nchi umiliki ardhi ni miaka 99 lakini Dodoma pekee ndio miaka 33.
Rais Magufuli alisema hata kama mabadiliko hayo yatasababisha kuvunjika kwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu(CDA) Dodoma, yeye yupo tayari.