The Senetor
Member
- Aug 23, 2014
- 41
- 23
Jana Rais Kikwete alisema muda wa kampeni za kuikubali au kuikataa katiba mpya bado haujafika na watu wasubiri muda ulioruhusiwa kisheria lakini anasahau yeye ndio wa kwanza kuvunja hiyo sheria maana amekuwa akiipigia kampeni kwa kuwaeleza wananchi kuwa ni nzuri na waipigie kura ya NDIYO mfano akiwa Tabora kwenye kufunga mbio za mwenge alisema katiba pendekezwa ni nzuri na wananchi waipigie kura ya ndio,iweje leo akiongea Warioba aseme anavunja sheria?Haya ni maneno yake ya jana
"Kwa sababu hiyo, nawaomba Watanzania wenzangu tuzingatie matakwa ya sheria ya kura ya maoni, ambayo imeelekeza vizuri lini kura ya maoni itafanyika, lini kampeni zitafanyika, lini wadau watatoa elimu, naomba tuwe na subira, tuizingatie sheria hii, tukiizingatia hii hakuna ugomvi, tume itakapotoa maelekezo ya utekelezaji wa fursa husika kwa wadau tuzitumie.
"Tukienda kinyume cha hapo ndiyo mnafika mahali mnagombana, wakati wa kampeni bado, wakati wa elimu kwa umma kwa mujibu wa sheria bado, sheria hii imezipanga siku, siku 60 kabla ya kura ya maoni, vyama vya kijamii na kiraia ruksa kuelimisha jamii, siku 30 kabla kufanya kampeni ya kuunga mkono ama kukataa, mwisho kura kama "ndiyo" imeshinda ama "hapana"," alisema Rais Kikwete. Kwa hiyo tumefika hapa tulipo kutokana na kauli za Rais Kikwete,narudia na tena namaanisha tumefika hapa tulipo kutokana na kauli za Rais Kikwete

Kikwete anaishusha hadhi taasisi ya urais !
Hebu chukulia alichoongea jana kwa mfano : Eti muda wa campaign bado na hivyo watu wafuate sheria !. Sheria ipi hiyo inayozuia watu wasiongee !?. Hivi unaweza ukawapa watu katiba inayopendekezwa ili waisome na kuielewa halafu utegemee hao watu wasiiongelee au kusema inafaa au haifai !? Wasipoelewa wakamuuliza mtu ili awaeleweshe ni makosa ? Mtu anayeona ana uelewa wa mambo hayo na akiamua (kwa gharama zake/au na za wanaomsupport) kuwaelimisha wale wanaotaka kuelemishwa ni makosa ?.
Elimu itakayotolewa na tume itakuwa rasimi, itakuwa na budget ya serikali na inategemea kuwa systematic and balanced, kwa maana kwamba itatolewa in such a way kwamba watu karibia wote wataelemishwa na kwa namna ambavyo itawafanya waweze kuelewa na kufanya maamuzi sahihi kama wanavyoona wao inafaa. Lakini hizi elimu nyingine ambazo sio rasimi hakuna mtu anayeweza kuzizuia kwani hakuna sheria yeyote inayovunjwa !. Wewe Kikwete inakuuma nini kama Jaji Warioba au mtu mwingine yeyote ameamua kutumia muda wake mwenyewe kuelimisha na mimi au mtu mwingine yeyote ameamua kutumia muda kumsikiliza ?.
Ni kweli, muda wa campaign bado lakini huo ni muda rasmi. Campaigns ambazo sio rasmi zinaendelea na hakuna namna mtu anaweza kuzizuia. Campaigns na uhuru wa kujieleza au kutoa maoni ni vitu ambavyo ni vigumu sana kuchora mstari kwamba hiki kinaishia hapa na hiki kinaanzia hapa !. Kwa kuthibitisha hilo Kikwete mwenyewe hapo hapo akiwa anasema muda wa campaign bado akafanya campaign kwa katiba inayopendekezwa kwa kusema tuipigie kura ya ndio kwani tukiipigia ya hapana tutakuwa tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele !. Kuzuia watu wasiongelee katiba ni sawasawa na kuzuia watu wasiongee !.
Simlaumu kwa kufanya campaign, ila hakutakiwa aseme hicho alichokisema, kwani tangu katiba inayopendekezwa itoke watu wengi sana including wa chama chake na yeye mwenyewe wamekuwa in full campaign mode !
Sasa anapokuja leo na kusema hivyo baada ya kuona watu wake wamezidiwa hoja, tumueleweje sisi ?. Je, kwa maneno haya, watu wakisema kwamba Kikwete ndie aliyemtuma Makonda na wahuni wenzake kwenda kuvuruga mdahalo uliokuwa unafanyika Ubungo Plaza wataonekana ni wazushi ?.
Cha ajabu Kikwete ameshindwa hata kukemea kitendo hicho cha aibu kilichofanywa na vijana wa chama chake !