Rais Kagame Kawaalika Yanga; Yanga yapeleka Taji Ikulu Rwanda

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797


Wednesday, 22 August 2012 12:33

0000000000000000kagamecuprwanda.jpg
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub (kulia) akiwa na Kombe la Kagame mkononi pamoja na Shadrack Nsajigwa wakiingia ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam tayari kwa safari ya kwenda Rwanda kwa ajili ya ziara ya kimichezo.Picha na Jackson Odoyo
Jessca Nangawe

MABINGWA wa Kombe la Kagame, Yanga ya Dar es Salaam, wamealikwa Ikulu ya Rwanda, ikiwa ni mara ya kwanza kwa klabu kutoka Tanzania kupata fursa kama hiyo.

Mbali na mwaliko huo, pia watakaporejea kutoka Kigali, watalipeleka kombe hilo, Ikulu Dar es Salaam baada ya kupata mwaliko kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete.

Yanga ilitwaa kwa mara ya pili mfululizo Kombe la Kagame baada ya kuifunga Azam FC 2-0 katika mchezo wa fainali wiki tatu zilizopita, Uwanja wa Taifa. Mwaka jana ilitwaa baada ya kuifunga Simba bao 1-0 kwenye uwanja huohuo.

Katibu Mkuu wa Yanga, Selestine Mwesigwa, alisema jana kuwa msafara wa timu hiyo utatinga Ikulu ya Rais Paul Kagame saa tano asubuhi leo hii.

Rais Kagame ndiye mdhamini mkuu wa michuano hiyo tangu mwaka 2002, ambapo amekuwa akitoa kiasi cha dola 60,000 kila mwaka kama zawadi kwa washindi.

"Kwa kuwa tumepata mwaliko kwenda Ikulu Kigali, tumeamua kubeba na taji letu kwa mdhamini wa mashindano," alisema Mwesigwa.

Mwesigwa alisema wakiwa nchini Rwanda pia watapata fursa ya kucheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa kujiandaa na Ligi Kuu Bara.

Wataanza kujipima nguvu na timu ya Polisi, kabla ya kuivaa Ryon Sports. Timu zote zimethibitisha kucheza mechi dhidi ya mabingwa hao wa Kagame.

Kuhusu mwaliko wa Rais Kikwete, Mwesigwa wamealikwa kwenda kula chakula cha jioni ambapo pia watakwenda na taji lao.

"Mheshimiwa Rais Kikwete ametualika kwenda kupata chakula pamoja naye mara baada ya kurejea nchini kutoka Rwanda," alisema Mwesigwa.

Katika hatua nyingine kocha mkuu wa Yanga, Tom Seintfiet amesema amefurahishwa na mabadiliko yaliyoonyeshwa na mshambuliaji Jerryson Tegete.

Tegete alitajwa na Sentifiet kama miongoni mwa wale ambao walistahili kuondoka Jangwani kutokana na kutomridhisha.

Akizungumza mara baada ya pambano la kirafiki dhidi ya African Lyon, Seintfiet alisema amefurahishwa kuona kadri muda unavyokwenda ndivyo Tegete anavyobadilika kwa kasi.

Tegete alifunga bao moja katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Lyon ikiwa ni mechi ya maandalizi kabla ya kuanza michuano ya Ligi Kuu Bara baadaye mwezi ujao.
 
Good Sporty-Politics...

US President anafanya kwa kila TIMU BINGWA USA kutembelea WHITE HOUSE; Sasa JK KIKWETE kaona AIBU na Sasa awaita YANGA, LINI Viongozi wa CCM walikuwa

Wastaarabu kupenda MICHEZO? Hawajali ndio Maana Olympics wachezaji 7; Viongozi 20;

KAGAME anaonyesha JINSI ya UPENDO wa MICHEZO YANGA wameshinda MARA 2; Hawajaitwa IKULU Dar Mpaka KAGAME kufanya Hivyo...

* NA MA MODS watarusha hii habari kwenye SPORTS na badala ya kuacha kwenye SIASA kuwa fundisho kwa WANASIASA wa CCM, CHADEMA, CUF, NCCR na

wengine
 
Hii nayo siasa kweli? basi peleka jukwaa la hoja mchanganyiko angalau itasound kidogo. Ni maelekezo tuu mwanajamvi mwenzangu.
 
Hii nayo siasa kweli? basi peleka jukwaa la hoja mchanganyiko angalau itasound kidogo. Ni maelekezo tuu mwanajamvi mwenzangu.

Uh Lalala... kwani sio za kisiasa na Michezo? au Mpaka usikie DINI na SIASA?
 
Good Sporty-Politics...

US President anafanya kwa kila TIMU BINGWA USA kutembelea WHITE HOUSE; Sasa JK KIKWETE kaona AIBU na Sasa awaita YANGA, LINI Viongozi wa CCM walikuwa

Wastaarabu kupenda MICHEZO? Hawajali ndio Maana Olympics wachezaji 7; Viongozi 20;

KAGAME anaonyesha JINSI ya UPENDO wa MICHEZO YANGA wameshinda MARA 2; Hawajaitwa IKULU Dar Mpaka KAGAME kufanya Hivyo...

* NA MA MODS watarusha hii habari kwenye SPORTS na badala ya kuacha kwenye SIASA kuwa fundisho kwa WANASIASA wa CCM, CHADEMA, CUF, NCCR na

wengine

Mkuu naona unatoa mapointi tu. Lakini kikubwa mkubwa ni kutokuwa bias katika kuamua. Huwa nashangaa sana kusikia wasanii wa ubongo wa fleva wanaingia kwenye jengo letu wakati wanachoimba ni kitu cha kawaida tu. Naskika BWM alimpatia Feruzi gari kutokana na wimbo wake wa Ukimwi. Hapo sawa. Lakini siyo hizi zingine.
 
Naona naota lakini nisaidieni kidogo.Yusuf Manji,mtoto wa kigogo kawachinjia Simba baharini mpaka Rage katoa mchozi,Kagoda,EPA na Mkulu.
Naona kuna jambo.
 


Rais Kagame akizungumza na Mwenyekiti wa Yanga, Manji




Rais Kagame akizungumza na Yanga



Sief Ahmad Magari akimkabidhi jezi ya Yanga Rais Kagame mbele ya Mama Fatma Karume



Mwenyekiti wa Yanga, Yussufr Manji akizungumza kitu mbele ya rais Kagame





Rais Kagame akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Yanga, Mama Fatma Karume



Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' akiwa na kocha Saintfiet, wakimkabidhi Kombe Rais Kagame




progress.gif
Edit Post Reply Reply With Quote
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom