pierre buyoya
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 476
- 163
Jina la John Pombe Magufuli sio jina geni kwenye siasa za Tanzania kama wanavyodhani baadhi ya watu wengi walioanza kufatilia siasa (active politics) mwaka jana kipindi cha uchaguzi mkuu. John Magufuli anliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1995 wakati huo Rais wa JMT alikuwa Mhe. Benjamin W. Mkapa. Akiwa mbunge kijana kutoka Biharamuro mashariki John Magufuli aliwahi kuwa naibu waziri akiteuliwa na Rais Mkapa na baadaye kuwa waziri kamili.
KWANINI JOHN MAGUFULI AMEKUWA RAIS AKIWA WAZIRI WA MARAIS WENGINE
Mwaka 1995 na 2000 Rais mstaafu wa awamu ya 3 Mhe. Mkapa alitoa ahadi nyingi sana wakati wa kampeni ambazo zilikuwa zikionesha wazi njia za maendeleo na ujio wa Tanzania Mpya, Lakini katika baraza zima la mawaziri Waziri magufuli alikuwa wazi kuwa ni mfanyakazi aliyebeba kwa kiwango kikubwa serikali ya awamu ya 3, Ahadi ya wananchi wa mtwara kutembea kwa Taxi kutoka Mtwara mpaka bukoba ilitolewa na Waziri magufuli na Sasandoto hiyo imetimia.
Awamu ya 4 iliyoongoza na Rais mstaafu Mzee Jakaya kikwete imekuwa ni awamu inayoshutumiwa sana kwa uzembe wa ufatiliaji lakini ni wazi kabisa katika kichaka kikubwa cha awazembe alikuwako mtu mmoja tu Dkt. John magufuli aliyeweza kufanya kazi iliyoonekana juhudi zake za kutandika wavu wa lami nchi nzima na wakati fulani alikuwa waziri wa uvuvi na kuinua sana sekta hiyo . . .
ITAENDELEA.....