Rais Hassan Rouhani: Nguvu za Iran haziko dhidi ya majirani na nchi za Kiislamu

Sinoni

JF-Expert Member
May 16, 2011
6,191
10,674
4bk478d9b4271b67t4_620C350.jpg

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, nguvu na uwezo wa Iran hauko dhidi ya majirani na nchi za ulimwengu wa Kiislamu.
Rais Rouhani ameyasema hayo asubuhi ya leo katika maadhimisho ya Siku ya Jeshi na kuongeza kuwa, kwa mujibu wa amri na wasia wa Imam Khomeini (ra) na kwa tadbiri na uongozi wa amiri jeshi mkuu wa majeshi yote, jeshi la Iran ni jeshi la Uislamu, ni jeshi la mfumo wa Kiislamu na jeshi la wananchi wote wa Iran.

Amesema hii leo taifa la Iran lina jeshi lenye nguvu, uwezo, misukumo ya kidini, Kiislamu na ni jeshi ambalo linafikiria maslahi ya kitaifa ya nchi.

Rais wa Iran amesema kuwa, kama leo watu wanaona madola makubwa ya kibeberu na vibaraka wake katika Mashariki ya Kati hawawezi kuitazama Iran kwa jicho la tamaa na usaliti ni kutokana na kuweko jeshi lenye nguvu na uwezo.

Rais Hassan Rouhani amesema pia katika maadhimisho hayo ya Siku ya Jeshi hapa nchini kwamba, jeshi la nchi hii litakata mikono ya wavamizi endapo watainyoosha kwa ajili ya maslahi ya taifa hili.

Ikumbukwe kuwa, Jumapili ya leo tarehe 17 Aprili inasadifiana na maadhimisho ya Siku ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu. Katika maadhimisho ya leo kumefanyika magwaride na maonyesho mbalimbali ya silaha ambayo yamehudhuriwa na makamanda wa ngazi za juu wa jeshi hapa nchini.

Chanzo: BBC
 
Iran mko vizur israel wakijaribu wataangamia
Pole Sana dada yangu Kwa kutokuwa na maarifa ya kuelewa, hakuna taifa Middle East la kuweza kuipiga Israel, Israel siyo taifa la kawaida Kama ambavyo akili yako inawaza ,Tatizo mpo kishabiki zaidi kuliko uhalisia, performance ya Israel ktk Vita na military operations mbalimbali Israel ipo juu Sana kuliko Iran ,je? unakumbuka six days war? Iran asingeshinda Vita ile, unaikumbuka Operation thunder at Entebe iliyochukua dk 90 Kwa mateka tisini na wote wakaokolewa Kasoro mama mmoja aliyekuwa hospital na mdogo wake Netanyahu, Yoni Netanyahu aliyekuwa kamanda wa kikosi cha makomandoo cha Sayaret matikal kuuawa ktk mission Iran hawezi kuja Africa na kukomboa watu wake .na hiyo ilikuwa mwaka 1976.
Nina mengi ya kukueleza kuhusu Israel, ila ondoa ushabiki na usimame ktk haki, ni Israel ikitumia shirika lake la kijasusi MOSSAD ndo imeua wanasayansi wengi wa nyuklia wa Iran, tena ndani ya ardhi ya Iran, Iran ameua wanasayansi wangapi wa Israel?
dadangu achana kabisa na hili taifa, hii nitakuja kuleta thread maalumu kuhusu hili, shirika la kijasusi la Israel la MOSSAD, ndo linaongoza duniani Kwa ubora kuliko hata CIA, Iran ana shirika gani la kijasusi mahiri?
MOSSAD ni hatari Sana, tulia ujue mambo dadangu.
 
mossad ovyo kabisa mbona mara kibao wanazidiwa akili na wafilisti????mbona wana riadha wao waliuliwa ka kuku keenye olimpic??
iran ina miaka 3000 pale middle east halijawahi guswa...waulize wamongolia walishindwa kwenye ardhi ipi har-megido
 
Huyu jamaa nishamsoma anachuki na wasomi (IRAN) yeye kila day israel tu hata kams uwezo huo hawana atalazimisha tuamini anachokisema
 
Tukiacha udini au ushabiki unavyoongelea Israel sio kama wao tu ukimpiga Israel ni kama umempiga USA. Jamani history ni ndefu na Iran hilo analijuwa wazi kabisa. Siasa za ME ni complicated kabisa kinachosemwa hadharani sio kinachosemwa ndani. Iran maadui zake wakubwa ni waarabu sio Israel na waarabu wanawachukia wa Iran ukiondoa mashia. Kwa ufupi Iran hawezi kuthubutu kushambulia Israel itakuwa maafa makubwa sababu USA hatakaa kimya. Kuna silaha watu hawatumii zikija kutumiwa ni msiba. Mimi nimeshawahi kusikia ndege ikipiga tu sio mchezo sauti sasa likitua lile la baharini kama uko Magomeni zile nyumba za bati basi wataokota mabati baharini. Mungu atuepushe na haya mambo. Vile vibomu vya gongo la mboto tu walitembea na chupi mpaka Ilala. Tuache kushabikia vitu hivi.
 
Back
Top Bottom