Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Habari wanaJF,
Leo mjini Dodoma yalipo makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi kilifanyika kikao cha kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM ngazi ya Taifa na kudhihirisha zile tetesi kwamba taratibu Rais John Pombe Magufuli ameanza kukabidhiwa mikoba ya uenyekiti wa CCM na kumuacha Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akibakia kama mzee mshauri wa chama.
==========================================================
Hapa katika picha ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kushoto ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipowasili mkoani Dodoma kwa ajili ya kikao hicho cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakielekea kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU.
Chanzo: Michuzi
============================================
Kikao hiki kinajadili maandalizi ya mkutano mkuu maalumu, ambao unatarajiwa kufanyika Juni mjini Dodoma na katika mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ataachia ngazi na kumkabidhi Rais Dk. John Magufuli kama utamaduni wa CCM ulivyo katika kukabidhiana kijiti cha uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa pindi anapochaguliwa Rais mwingine wa Tanzania kutoka CCM.
Tangu wiki iliyopita vikao kadhaa vya Sekretarieti vimekuwa vikiendelea vikiwahusisha watendaji wa juu wa CCM pamoja na makatibu wa idara husika ambao huteuliwa na mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa nao wanaungana na viongozi wa ngazi za juu wa CCM katika kikao kwa mujibu wa Katiba ya CCM.
Katika kikao hiki kitajadili na kupitisha majina ya wajumbe 10 wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kutoka miongoni mwa wabunge wa CCM ambapo wabunge walioomba nafasi hizo, majina yao yatapelekwa kwa wabunge wa chama hicho kwa ajili ya kupigiwa kura.
Wabunge wana nafasi 10 za NEC na waliokuwa wajumbe walishapoteza sifa za kuwa wajumbe baada ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, hivyo kwa kawaida kila Bunge jipya linapochaguliwa ni lazima uchaguzi ufanyike.
Pamoja na kupitia majina ya wabunge waliojaza fomu, pia CC itajadili majina ya wabunge walioomba nafasi ya katibu wa wabunge wa CCM ambapo kuna wajumbe zaidi ya watatu wamejaza fomu.
Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM anayemaliza muda wake ni Mbunge wa Peramiho, Jenister Mhagama.