Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,859
Kufuatia kauli ya Rais Donald Trump wa Marekani kwamba utawala wake utawaweka mbele wamarekani zaidi kuliko wengineo, ni wazi kuwa Tanzania yuna jambo la kujifunza. Katika hotuba yake mara baada ya kuapishwa, Rais Trump 'aliponda' matumizi ya Marekani nchi za nje bila kuwajali kwanza wamarekani wenyewe.
Rais Trump, kupitia hotuba yake hiyo, ametuma ujumbe wa wazi kwa nchi nyinginezo ikiwemo Tanzania kuwa umefika wakati wa kutumia vyema futsa na rasilimali tulizonazo. Rais Trump ametutaka kufikiri zaidi na zaidi kuhusu kupata viongozi bora, sera bora, sheria bora na utekelezaji mzuri ili 'tujitegemee'.
Rais Trump, kwa miaka minne ya utawala wake, atasimamia alichokisema. Atasema na kufanya kile alichokiahidi kwenye kampeni zake na hata kwenye hotuba yake ninayoizungumzia hapa. Rais Trump wa Marekani atatulazimu watanzania kuchagua kwa ubora cha kufanya na namna ya kufanya tulichokichagua.
Wakati ule wa misaada ya kimaendeleo na kijamii unaelekea kukoma kwa haraka. Rais Donald Trump ameshatutumia ujumbe watanzania. Rasilimali zetu, tulizoziweka kwenye mikono ya Serikali yetu, zapaswa kutumiwa ipasavyo katika kutuneemesha wananchi wote na kwa maendeleo ya Tanzania yetu. Tunapaswa kufikiri zaidi na zaidi.