Rais Buhari atangaza utajiri wake

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,702
Reaction score
1,716



Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametangaza kuwa ana $150,000 (£100,000) kwenye akaunti zake za benki, katika hatua inayolenga kuendeleza uwazi na kupiga vita ufisadi serikalini.

Kiasi hicho kinaonyesha kuwa amekuwa akiishi "maisha ya kujinyima", msemaji wake Garba Shehu amesema.

Bw Buhari anamiliki makao matano na nyumba mbili za matope, pamoja na mashamba kadha, akaongeza.

Kiongozi huyo wa zamani wa kijeshi alichaguliwa kuwa rais mwezi Machi ahadi zake kuu zikiwa kukabiliana na ufisadi na ukosefu wa usalama.

Ufisadi ni tatizo sugu katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Afrika na mwezi uliopita, Bw Buhari alisema $150bn (£100bn) zimeporwa kutoka kwa hazina ya serikali.

Bw Shehu alisema kupitia taarifa kuwa Bw Buhari ana shamba la matunda na renchi yenye ng'ombe 270, kondoo 25, farasi watano na ndege wengi.

Pia anamiliki hisa katika kampuni tatu - Berger Paints, Union Bank na Skye Bank, taarifa hiyo iliongeza.

Hata hivyo, makamu wa rais wa Nigeria Yemi Osinbajo ni tajiri kumshinda mdosi wake.

Taarifa hiyo ilisema Bw Osinbajo ana $900,000 (£600,000) kwenye akaunti zake za benki.

Kwenye fomu ya kutangaza utajiri wake, Bw Osinbajo pia alifichua anamiliki nyumba nne, moja ikiwa ya vyumba viwili vya kulala ambayo analipia mkopo mjini Bedford, Uingereza.

Taarifa hiyo haikusema thamani halisi ya mali yote ya rais na makamu wake, ikieleza kuwa stakabadhi zilizokabidhiwa Afisi ya Maadili zitafanywa wazi kwa umma karibuni baada ya ukaguzi wake kukamilika.

Chanzo: BBC
 
Mmmh !! imposibo huyo labda siyo mNigeria... "vijisenti" hawa watu ni mBilioneaz!!
 
Nimeshangaa sana aisee...kuwa kiongozi mkubwa Wa jeshi miaka mingi.,..na menhine ambayo siyajui..eti ana Nyumba mbili, ana 150,000$, kondoo 25??? Teh teh teh...ingawa sijui ni vigumu kuamini.
 
Kama kawa karibu viongozi wote wa Africa wanafanana kwa usanii wao,huyu alipokuwa mtawala wa kijeshi alipiga sana hela. Unaambiwa pamoja Sani Abacha kufisadi hela nyingi lakini maendeleo na hali za wananchi zilikuwa nzuri kuliko viongozi wengine wote wawe wa Kiraia au wa Kijeshi.
 
Wasalaaam alleikum!!

Duru zenye kujuza zinasema kuwa Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria anawezekana ndiye Rais lofa kuliko marais wote wa Africa. Nyaraka za kuorodhesha mali zake ambazo alizirejesha katika kukidhi matakwa ya kisheria; na baadaye kuwekwa wazi zinaonyesha kuwa ana US $ 150,000 tu katika akaunti yake binafsi. Anamiliki nyumba tano za tofali za sement na nyumba mbili za tofali za matope, ana ngombe 250, kondoo 25, farasi watano na ndege wa kienyeji (chiriku, njiwa etc) kadhaa. Ameandikisha kuwa ana gari mbili alizonunua kutokana na akiba zake, na hana akaunti nje ya nchi, hana kiwanda, hana kampuni na wala hana kisima cha mafuta.

Huyu Rais amenifurahisha sana kwa uwazi alioonyesha kulinganisha na marais wengine katika Africa, mfano Jose Eduardo dos Santos wa Angola: $20 Billion, Uhuru Kenyatta wa Kenya: $500 Million, Paul Biya wa Cameroon: $200 Million, na King Mswati III wa Swaziland: $100 Million. Rais aliyemtangulia Goodluck Jonathan anazo: $100 Million.

====================================

Source: https://www.washingtonpost.com/news...as-leader-may-be-the-least-corrupt-in-africa/
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…