Rais atengeneze mkakati wa siri kushinda kesi za ufisadi

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,305
3,327
Licha ya juhudi kubwa ambayo mh Magufuli anayoionesha lakini bado kuna baadhi ya vyombo vinavyosimamia haki
vinamuangusha.

"Kwenye kesi ya samaki wa Magufuli DPP alinyofoa baadhi ya mashitaka ili serikali ishindwe".Raisi akaongeza
"Haiwezekani licha ya serikali kua na wanasheria mahiri lakini serikali imekua ikishindwa kesi".

Kwa kauli hizo raisi anathibitisha kwamba licha ya juhudi zinazo chukuliwa lakini mwisho wa siku yeye si mtoa haki.

Naamini raisi anapaswa kusimika kwa siri watu watiifu kwake kwenye mfumo mzima wa mahakama ili wasaidie taifa hili vinginevyo baadhi ya watoa haki wasio waaminifu watakwamisha juhudi za raisi.

Watu wachache wanaweza sababisha serikali kujikuta inawalipa fidia mafisadi baada ya kushindwa kesi ambazo haikupaswa ishindwe.
Najua hapa kutaanza habari ya watu kulalamika serikali kuingilia mahakama lakini kwa mazingira haya ambapo serikali inashindwa kesi hovyo kunahitajika umafia ili hii nchi isonge mbele.

Mh raisi yupo mbioni kuanzisha mahakama ya mafisadi hizi ni juhudi kubwa lakini kuna ulazima mh raisi akaandaa timu ya wanasheria watiifu kwake kuanzia majaji mpaka mahakimu ili kuhakikisha haki inatendeka.

Nasisitiza lengo si kukandamiza haki bali kuhakikisha haki inatendeka.
 
waafrica ni watu wapumbavu sana.Binafsi sioni umuhimu wa mahakama ya mafisadi zaidi ya kutaka kupoteza fedha nyingi tu kwenye maswala ambayo hayana tija.
Binafsi naona ni bora kutungwe sheria mpya,kuweka ufanisi wa kazi,kuboresha mishahara ya wafanyakazi na kujenga patriotism na ari kwa wananchi.
Pia,tukianza kutafuta mahakama ya mafisadi naomba sana tuondoe kinga za maraisi hapo ndipo nitawalewa kuwa katika hii vita kweli tuna maanisha.
pia ningeomba kwanza kikwete na mwanae wafikishwe mahakamani,wezi wa escrow,IPTL ,Mkapa and Co hawa wote wangefikishwa mahakamani kujibu makosa ya kuhujumu uchumi.
nasema tena,kama kweli tumedhamiria kupigana hii vita then MAGU AANZE hapo kama nilivyosema otherwise ni waste of time na uonevu,upuuzi na ujinga.
 
China na Korea Kaskazin ,huko unanyongwa tuu hata kesi hamna, mbona fisadi anajulikana tuu, mi nashangaa kesi za bongo

Kama wake samaki wa magufuli walitushinda utasema kuna kitu apa!!!
 
Kwa hali inayoendelea sasa nahisi ushauri wangu umesikika kama!
Zamani wabunge kufanya vurugu ilikua jambo la kawaida kabisa na wakipelekwa mahakamani kesi wanashinda tu lakini leo wanaipata wanapigwa nyundo.
 
Back
Top Bottom