Rais anapokuwa kibaka, Mutharika na maburungutu ya pesa uvunguni mwa kitanda!

Huyu kafundishwa ni kina Mkapa ambao hadi Ardhi zenye madini wamejimilikishia kama kule muheza na Kiwira,
 
Kinachosikitisha sana ni upofu na kujuana hata kwa hawa waliomrithi mfalme Mutharika. Maana wameishasema eti mazishi yake yatamkamua Mmalawi maskini si chini ya kwacha 150,000,000. Alipaswa azikwe kwa pesa yake mwenyewe. Hilo hekalu hakuna shaka litaanza kuhudumiwa kwa pesa ya walipa kodi hao hao aliowaibia. Wizi ndani ya wizi alijisemea Remmy Ongala. Hamuoni Lowassa anavyolipwa pesa ya kustaafu wakati hakustaafu ukiachia mbali kutuachia balaa la mgao na ulanguzi wa umeme? Nani atamwajibisha nani iwapo samaki wote wana masharubu huku ngedere wote wakiwa wezi wa mahindi? Ama kweli kesi ya nyani mpelekee ngedere haki itatendeka kwa mahindi.
 
Huyu kafundishwa ni kina Mkapa ambao hadi Ardhi zenye madini wamejimilikishia kama kule muheza na Kiwira,

Mkuu STEIN, tafadhari usinikumbushe juu ya kumbakumba huyo!!! katiba ya Tz inampa kiburi sana, kama angeishi milele, mimi ningejinyonga hadi nife.
 
Hilo Ndata farm lenyewe lilikuwa na eneo kubwa balaa - japo miaka ya mwishoni alikata sehemu akatoa eti "zawadi" kwa Malawi na hapo kinajengwa chuo kikuu cha sayansi na teknilojia.
 
Haya bhana ila sijui bongo tukianza kuwasachi itakuaje maana waziri anakutwa na four milioni za matembezi

wametofautiana kidogo tu, mmoja anaficha chini ya kitanda na kutaka ziwe nyingi, mwingine anaenda nazo night club kuringishia mademu..
 
Bora mkulu wetu anazipeleka kila wiki kwenye zile nyumba mbvofu mbofu mpaka ufikirie kuzifwata hata uwe poliisi unahisi roho yako itakuwa halali yao
 

Hawa wtu wengine hawa hakukuwa na sababu hata ya kufanya state funeral. Wangeenda zao taratibu tu. Imagine he wanted his young brother to take over after ending up his official terms. Alikuwa anafikiria yeye ni nani?
 
Hakuwa transparent, ndio maana watu walikuwa wanampinga kwa ufisadi lakini ni mchumi aliyebobea ndio maana alificha hela kwenye begi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…