Rais anapokuwa kibaka, Mutharika na maburungutu ya pesa uvunguni mwa kitanda!

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
[h=3]Mutharika, kurithishana na maburungutu ya dola[/h]Chanzo: www.mpayukaji.blogspot.com

UROHO NA UNAFIKI WA MARAIS WETU

thumbnail.aspx
suitcase_468x269_to_468x312.jpg

Habari zilizoripotiwa na gazeti la Nyasa Times ni kwamba mabegi na masanduku yaliyojaa pesa yalikutwa kwenye chumba cha rais wa zamani wa nchi hiyo marehemu Bingu wa Mutharika. Habari zinaendelea kusema kuwa pesa hiyo ilikamatwa na polisi baada ya kugundua kuwa ndugu wa marehemu walikuwa wakipanga kuihamisha pamoja na mali nyingine za serikali. Ni aibu kiasi gani. kwanza kwa rais kuficha pesa uvunguni mwa kitanda tena kwenye karne ya 21?

Ni aibu kiasi gani kitendo hiki kinapotendwa na rais tena msomi aliyebobea katika uchumi? Je huyu rais alikuwa ameelimika kweli? Je ni watawala wangapi wa kiafrika ni aina ya Mutharika? Je wanajifunza nini ingawa uwezo wao wa kujifunza siku zote ni mdogo? Muhimu ni kuwaambia wazi kuwa kila mficha maradhi kilio kitamfichua kama ilivyotokea kwa Mutharika. Ajabu wakati rais akilalia mamilioni ya dola na kwacha, mamilioni ya watu wasio na hatia wanakufa kwa magonjwa yanayotibika! Je namna hii kuna haja ya kuwa na rais ambaye kimsingi ni mwizi anayeitwa mheshimiwa? Kama rais wa nchi maskini kama Malawi isiyo na raslimali za kutosha anakutwa na mamilioni ya dola uvunguni mwa kitanda hao marais wa nchi zenye raslimali nyingi kama DRC na Tanzania wanalilia mabilioni kiasi gani? Kwa habari zaidiBONYEZA HAPA.
 
Haha, viongozi wa Africa bwana...
Huwa hawaridhiki.

1)Wanajipangia mishahara na marupurupu mengi kuliko hata baadhi ya ma_raisi wa ulaya.. Lakini bado wezi wa mali za umma.

Uliza hapa Tanzania, viongozi wetu wana_share kwenye migodi kiasi gani... Unaweza ukakimbiaaaa...

2) Ndo maana wengi wanakufa kwa aibu. Kutokana na uroho wao. (Gadaffi, Mobutu, n.k).

Na sina uhakika kama hizo hela wakifa, wanaondoka nazo, au wanaziacha hapa hapa ardhini.

NOTE: Umaskini wa afrika, asilimia kubwa unachangiwa na viongozi wao.
 
Wakiingia madarakani hwawtumii tena bongo zao kwa kuileteanchi maendeleo ila wanawaza namna ya kushinda uchaguzi mwingine na kujipatia pesa pasipo kufanya kazi.
 
ndio maana wanachakachua kura wakati wa uchaguzi

Haha, viongozi wa Africa bwana... Huwa hawaridhiki. 1)Wanajipangia mishahara na marupurupu mengi kuliko hata baadhi ya ma_raisi wa ulaya.. Lakini bado wezi wa mali za umma. Uliza hapa Tanzania, viongozi wetu wana_share kwenye migodi kiasi gani... Unaweza ukakimbiaaaa... 2) Ndo maana wengi wanakufa kwa aibu. Kutokana na uroho wao. (Gadaffi, Mobutu, n.k). Na sina uhakika kama hizo hela wakifa, wanaondoka nazo, au wanaziacha hapa hapa ardhini. NOTE: Umaskini wa afrika, asilimia kubwa unachangiwa na viongozi wao.
 
Rafiki yangu Ben wa Saanane alisema kwamba Afrika tumepoteza mwana mapinduzi ... nilimpinga sana kwa kuwa siku hizi Afrika hatuna wana mapinduzi ila tuna mafisadi. Wanamapinduzi bado wako Korea na Cuba, maana hata wakifanya ufisadi, hawawezi kwenda kuwekeza nje ya nchi kwa kuwa walishajifungia ndani.

Viongozi wengi wanaokataa IMF na WB, wanatumia mgongo wa kupinga ubeberu na kumbe wanaogopa wakiwakaribisha watakuwa wanawachungulia kwa karibu ili kuona nyendo zao. Sasa akina Bob na Bingu (RIP) hawakutaka wachunguzwe maana ni rahisi siri zao kuvujishwa na hivyo kuongeza migogoro ya ndani ya nchi, na nchi inakuwa haitawaliki tena. Ukienda Zimbabwe hakuna ambaye huwa anahoji Mugabe ana bei gani nje ya nchi.

Ukisoma news iliyo kwenye hii link hapa nchini ndo utachoka kabisa. Ndipo unapoelewa kwanini Mugabe ameguswa sana na msiba huu wa Bingu. Hata kama tuhuma hizi zina ukweli kwa robo tu, then ni hatari kubwa. Hawa ndo wanamapinduzi wetu kiboko cha mabeberu, lakini mafisadi waliokubuhu ambao wako tayari kufanya kufuru huku wananchi wao wakipoteza maisha.

Wa Mutharika
 
..Kwa hio siku hizi hawapeleki tena kuzificha ktk Benki za Uswisi. Siku hizi wanaficha chini ya kitanda. Damn African Leaders.
Hawapeleki, wanaogopa International Transparecy. Hata akina jamaa wa Ben Ali na Hosni Mubaraka walikamatwa wanataka kutoa nje ya nchi dhahabu kwa tani na mabiloni ya fedha. Ni aibu kwa kiongozi lakini ni sifa kwa mtawala.
 
Nikiwa rais nachonga kabisa sanduku lachuma chuma, naweka chini ya kitanda ndiyo itakuwa benki yangu

ha ha ha ha:A S kiss:
 
Mimi nilishaacha kumuita kiongozi yeyote mheshimiwa,baada ya kugundua kwamba hawana chochote cha kuwafanya waheshimike.Infact ni vibaka tu ambao wanastahili kufungwa matairi na kuchomwa.

Back
Top Bottom