iparamasa
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 13,437
- 14,924
Taifa la Tanzania tangu Uhuru halijazoea kuona kiongozi Mkuu akipewa nafasi ya kuongea kanisani au nje ya kanisa baada ya yeye kuhudhuria ibada.Msingi wa hii ni kwamba nchi hii ina watu wa dini tofauti,waislam,wakristo,wapagani,wahindu. Si kila mahali Rais anaweza kuingia na kutoa kauli au hotuba,mfano msikitini au kwenye temple za mabudha,hawa watajisikia unyonge endapo kila Jumapili watalazimika kuangalia ibada fulani ili wamuone Rais kwenye TV akitoa kauli.
Nashauri atumie forum nyingi tu ambazo taifa limempa ili awasiliane nalo, hii inaweza kuepushwa kwa kuzuia waandishi wa habari kuandamana naye na wamuache yeye na waumini wenzie watulize nyoyo zao na wawe na amani ya kuwasiliana na mwenyezi Mungu kuliko kuwafanya waumini wawe wanazungusha macho kuwaangalia waandishi wa habari wakiwa na makamera makubwa makubwa.
Waandishi wa habari pia mumuache Rais ahudhurie ibada kwa amani na msiwape unyonge watu wa dini nyingine.