Ndugu wanajamvi,
Nchi yetu Tanzania mwaka huu 2015 tutakuwa na uchaguzi mkuu wa uongozi wa nchi hii.
Moja ya nafasi nyeti kabisa ni pale tunapotakiwa kumpata kiongozi mkuu/rais wa nchi.
Kwa sasa vyama vyote vya siasa vipo kwenye mchakato wa kuona ni nani ndani ya chama husika atafaa kuteuliwa miongoni mwa wanachama wao kupeperusha bendera ya chama husika ktk kinyang'anyiro hicho cha kumpata rais wa nchi.
Kwa sasa tayari wengine wameenda mbali kwa kuanza kutamka majina ya wanaoonekana kufaa kupewa dhamana ya kuliongoza taifa hili.
Baada ya kutafakari sana, miye naona labda kwa kuwa sasa tunayafahamu masuala/changamoto zinazolikabiri taifa hili ikiwamo ufisadi uliokithiri, hakuna uwajibikaji, rushwa kubwakubwa, wananchi hawafanyi kazi/hawajitumi, hakuna uadilifu kwa viongozi lakini na kwa jamii kwa ujumla wake, wananchi kuchukulia mambo kwa kawaida sana, viongozi waliopewa dhamana na wananchi kuwa waongowaongo, viongozi kutoa ahadi zisizotimilika (hasa wakati wa kampeni) na mengine mengi yanayofanana na hayo.
Kwa hali ilivyo nchini hapa ni muda muafaka sasa kwetu watanzania/wapiga kura kuanza kutafakari ni kiongozi mwenye sifa zipi tunaye muhitaji kuliongoza taifa hili.
Kwa changamoto zinazilikabiri taifa hili, hiki si kipindi cha kumpendekeza ama kuzungumzia mtanzania anayefaa kupewa dhamana ya kuliongoza taifa hili kwa kuangalia mwonekano wake, sura yake, umri wake, anatoka upande gani wa nchi na mambo mengine yanayofanana na hayo.
Hebu tusaidianeni kupata sifa za mtanzania anayefaa kupewa dhamana ya kuliongoza taifa hili hapa chini.
Miye naanza na sifa hizi;
1. Mchapa kazi (hii ije na kumbukumbu za nini aliwahi kulifanyia taifa hili)
2. Mwadilifu
3. Asiwe mpole sana au mkali sana
4.Mwajibikaji (hii iendane na kumbukumbu za utendaji wake, kuwa kama ndani ya utendaji wake aliwahi kuwa kwenye mazingira yaliyokuwa yanamsababishia kuwajibika na hakuwa tayari kuwajibika ama aliwajibika kwa kulazimishwa, huyu hatatufaa)
5. ............