Rais ajaye atenganishe Elimu na Siasa

Rais ajaye atenganishe Elimu na Siasa

Joined
Jul 9, 2014
Posts
64
Reaction score
9
Sijui nini kinaendelea katika mfumo wa elimu yetu isipokua ninachokiona ni kuwa,

Tunahitaji kiongozi ambaye hatatumia sekta ya elimu kama mtaji wake kisiasa,

Aheshimu na kuwatumia wataalam na wadau wa elimu kabla na baada ya kufanya maboresho yoyote katika mfumo wa elimu.

Asiyumbishwe na wanasiasa bali awe na falsafa isiyotetereka ili kuokoa elimu yetu.

Sekta ya elimu isijazwe walipwa 'fadhila'...kwani hata kama watakua wataalam wabobezi bado watakua pale kwa sababu ya fadhila.

Kiongozi ajaye atuondolee utata wa 'ipi falsafa ya elimu yetu?'

Kiongozi ajaye afaham kuwa akifanikiwa kuitendea haki sekta ya elimu...atatambulika kama 'Mzalendo.'

Niwaombe tu watanzania wenzangu tusisubiri kampeni kuanzia sasa tuone nan ana moyo wa dhati na uchungu na elimu ya nchi hii....

nimalizie tu kwa kumnukuu hayati baba wa taifa na mwasisi wa 'falsafa ya elimu ya ujamaa na kujitegemea'...nanukuu,"HAKUNA UMASKINI MBAYA KAMA UMASKINI WA MAWAZO NI UMASKINI MBAYA SANA!"

Wanafalsafa wakongwe kama akina Plato, Dewey, Roussseau,LutherKing na Nyerere walieleza elimu bora ni ile inayoweza kufanikisha haya katika maisha ya mtu binafsi na jamii yake.

" Liberation, Self Reliance and Development"

Elimu si siasa...ingawa tunahitaji wanasiasa safi kupata elimu bora
 
Back
Top Bottom