Raia Mwema limewatambua wasiotaka kumkabidhi uenyekiti Magufuli

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
15,502
22,355
UENYEKITI CCM

magu_4.jpg

Magufuli atikiswa.

Hii habari ni kutoka katika gazeti la Raia Mwema, toleo la 461 la tarehe 8 Juni 2016

Vigogo wapanga kumpindua

SASA ni rasmi kwamba kuna vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanajipanga kuzuia Rais John Magufuli asiwe Mwenyekiti wa chama hicho baadaye mwaka huu kama inavyotarajiwa na wengi, Raia Mwema limeambiwa.

Gazeti hili limeambiwa kwamba mkakati huo unapangwa kwa siri kubwa na kwamba utatekelezwa wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi ujao.

Vyanzo vya kuaminika vya gazeti hili vimeeleza kuwa kuna wajumbe ambao watasimama na kutoa hoja kwamba si lazima kwa Mwenyekiti wa CCM kuwa pia Rais kutokana na sababu mbalimbali.

“Kuna sababu kadhaa ambazo zitatumika. Kwa mfano, kuna watakaosema kwamba dunia nzima hivi sasa mfumo huo hautumiki. Nchi zinazotajwa kutotumia mfano huo ni Kenya, Afrika Kusini na hata Marekani.

“Hoja itakuja kwamba kazi za chama ni za chama na za serikali ni za serikali. Wataeleza kuwa Jacob Zuma (Rais wa Afrika Kusini) si Rais wa chama tawala (ANC). Rais wake anaitwa Baleka Mbeke.

“ Kuna wengine watatoa hoja kwamba katika hali ya sasa, kama Rais akichukiwa, basi na chama kitachukiwa pia kama mtu mmoja atashika nafasi hizo mbili.

Ni muhimu chama kiokoe serikali au serikali iokoe chama na si wote wazame kwa pamoja,” kilieleza chanzo hicho ambacho ni mmoja wa wanachama waandamizi wa CCM waliowahi kushika nyadhifa za juu serikalini.

Hata hivyo, mtoa habari wetu huyu ambaye aliomba kutotajwa jina kwa maelezo kuwa wahusika ni watu anaofahamiana nao vizuri; alisema kwamba ni wazi Rais Magufuli ana taarifa hizo na kwa vyovyote atajiandaa kupambana na hali hiyo.

Mmoja wa vigogo wanaotajwa kuhusika na mpango huu aliliambia gazeti hili kwenye mahojiano naye yaliyofanyika Dar es Salaam kuwa haoni kama ni tatizo kama kuna wana CCM wanaoamini kuwa utaratibu wa Mwenyekiti wa chama kuwa pia Rais wa nchi umepitwa na wakati.

“ Sikiliza, mimi sitaki unitaje jina kwenye gazeti lako kwa sababu ukifanya hivyo utakuwa tayari umenihukumu kwamba nimo kwenye huo mpango. Mimi sijui chochote.

“Hata hivyo, sidhani kama wanaofikiri tofauti wanakosea. Kama wataibua hoja hiyo, itapewa majibu na huo ndiyo utaratibu wetu ndani ya CCM.

“Kama watu wanaona kwamba kitu kimepitwa na wakati watasema tu. Tulikuwa na Azimio la Arusha baadaye likabadilishwa. Tulikuwa tumekataza wafanyabiashara kwenye siasa lakini baadaye tukawarudisha na sasa tunafikiria kuwatenganisha na siasa. Hayo yote ni mawazo”, alisema kigogo huyo ambaye ni mwanasiasa maarufu wa CCM ambaye aliwania urais na Magufuli katika mchakato wa ndani wa CCM mwaka jana.

Katika miaka ya 1990, aliyewahi kuwa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kuwaambia wanachama wa chama hicho kuwa ni muhimu kwa mtu mmoja kushika nyadhifa zote hizo kwa sababu ya umoja na utengamano ndani ya chama.

“ Mnaweza kuamua kuwa na Rais mtu mwingine na Mwenyekiti wa chama. Lakini omba Mungu wapatane maana wasipopatana itakuwa vurugu tupu,” Mwalimu alinukuliwa kusema wakati huo.
Katika historia ya CCM, ni Mwalimu pekee aliyepata bahati ya kuwa Mwenyekiti wa chama wakati Rais wa Tanzania akiwa Ali Hassan Mwinyi, lakini wanasiasa wakongwe kama Pius Msekwa wanaamini kuwa isingekuwa rahisi kwa Nyerere kuondoka ghafla madarakani kwa kuacha nyadhifa zake zote.

Katika mahojiano yake aliyowahi kufanya na gazeti hili nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Msekwa alisema kwamba anaamini Mwenyekiti wa sasa wa CCM, Jakaya Kikwete, atamuachia Magufuli wadhifa huo mapema.

“Katika historia ya Tanzania, ni Nyerere pekee ndiye aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM kwa muda mrefu huku mzee Mwinyi akiwa Rais. Lakini kulikuwa na sababu wakati huo kwamba Watanzania walikuwa wakimpenda sana Mwalimu na nchi ingetikisika kama angeachia nyadhifa zote mbili,” alisema Msekwa mapema mwaka huu.

Wakati gazeti hili likiwa na taarifa kwamba baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu huo tayari wameanza kutumiwa mialiko ya kwenda kuhudhuria mkutano huo, kuna wajumbe wameanza kudai kwamba mkutano huo ‘hautanoga’ kufanyika wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ulioanza wiki hii.

Raia Mwema limeambiwa kwamba sababu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mojawapo ya zile zinazoanza kuibuka sasa kutaka Mkutano Mkuu wa CCM usogezwe mbele, baada ya ile ya zamani ya ukosefu wa fedha kuonekana haina nguvu.

Gazeti hili limeambiwa kwamba baada ya viongozi wa CCM sasa kudai kwamba kuna matatizo ya kifedha, Magufuli mwenyewe ameamua kubeba mzigo wa kuhakikisha fedha zinapatikana kufanikisha hilo.

Mkutano huo unaweza kufanyika baada ya Bunge la Bajeti kumaliza mkutano wake mjini Dodoma mwishoni mwa mwezi huu ili kuwezesha wale watakaokuwa Dodoma kutohangaishwa kurejea makwao na kisha Dodoma tena kwenye mkutano huo.

Alipoulizwa na Raia Mwema kuhusu kama Magufuli amekubali kubeba mzigo wa kutafuta fedha za Mkutano Mkuu huo wa CCM na mambo mengine yanayohusu Uenyekiti wa CCM, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, alisema hana mamlaka ya kuzungumzia mambo ya chama.

“ Mambo ya CCM mimi yako nje ya uwezo wangu. Siwezi kukujibu ndugu yangu naomba tu uwaulize wenyewe kwa vile mimi niko serikalini na kwenye chama wana watu wao”, alisema.
Juhudi za kumpata Msemaji wa CCM, Christopher ole Sendeka, kuzungumza kuhusu suala hili hazikufanikiwa hadi tunakwenda mitamboni kwa vile ofisini kwake alielezwa kuwa yuko safarini kwenye mikoa ya Kusini na simu yake ilikuwa haipatikani.

My Take:

Vita ni kubwa sana ambayo raisi wetu Magufuli ameamua kuivalia njuga, na hata hili la mchungaji Gwajima ambae jana kutoa ujumbe wake kwa raisi Magufuli na "YULE", halijatoka bure.

Na hao wanachama wawili waandamizi wanaotajwa hapo kushiriki hii blackmail ni akina nani hao?

Raia Mwema nakuaminieni katika ubora wa taarifa zenu za uchunguzi.

Mzee Pius Msekwa na wazee wenzio kiokoeni chama hiki.

Watanzania tunakwenda wapi?
 
Hoja itakuja kwamba kazi za chama ni za chama na za serikali ni za serikali. Wataeleza kuwa Jacob Zuma (Rais wa Afrika Kusini) si Rais wa chama tawala (ANC). Rais wake anaitwa Baleka Mbeke.
Hawa waandishi wa habari nao wawe wanafanya home work zao kwanza!! Zuma ni Rais wa chama Baleka ni Mwenyekiti!!

Rais wa chama ANC ndiye mwenye nguvu zaidi. Ndiyo maana Mbeki alipooteza hiyo nafasi waliweza kum-recall na kupoteza cheo chake cha Ukuu wa nchi.

Nchi nyingi tu za kiafrika bado zinatumia huu mfumo wa CCM na Tanzania including Zambia, Uganda, Malawi, Rwanda, Namibia n.k.
 
Tunasubiri mjumbe huyo ataesimama na hoja hiyo tuone! Manaa JPM ameshajua nani wako behind ya hiyo kitu ili kumpung nguvu na kumfanya asiguse interest zao!

Inajulikana!! Ndio maana safari za Ikulu kwa mstaafu mmoja haziishi....akienda na mstaafu mwingine nae anaitwa!! Nadhani balance mkwara
 
Hawa waandishi wa habari nao wawe wanafanya home work zao kwanza!! Zuma ni Rais wa chama Baleka ni Mwenyekiti!!

Rais wa chama ANC ndiye mwenye nguvu zaidi. Ndiyo maana Mbeki alipooteza hiyo nafasi waliweza kum-recall na kupoteza cheo chake cha Ukuu wa nchi.

Nchi nyingi tu za kiafrika bado zinatumia huu mfumo wa CCM na Tanzania including Zambia, Uganda, Malawi, Rwanda, Namibia n.k.

Hapa ndipo wanapowachanganya wasomaji wao.
 
MBONA EL, ILIPOSEMEKANA ALITAKIWA KUPEWA UENYEKITI WAPAMBE WA JK WALING'AKA?....KUMBE MKUKI KWA NGURUWE EE,,,,

Wadhifa wa uenyekiti CCM una malengo mapana zaidi- unatumiwa kwa manufaa binafsi.

Hivyo kunakuwa na mgongano wa kimaslahi.

Ila haya yote yasingeweza kutokea wakati wa hayati Mwalimu Nyerere akiwa hai.
 
NGOJA WAVURUGANE.....YETU MACHO...
 
Kale ka uwimbo ka ccm nani anako anitumie.

Tumeipenda wenyewe ndii ndiiii
Wacha wavimbe na wapasukee ndii ndii

Wacha waisome namba eeeeh , ccm mbele kwa mbele.

Mwaka huu magamba yatawapwaya
 
UENYEKITI CCM

magu_4.jpg

Magufuli atikiswa.

Hii habari ni kutoka katika gazeti la Raia Mwema, toleo la 461 la tarehe 8 Juni 2016

Vigogo wapanga kumpindua

SASA ni rasmi kwamba kuna vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanajipanga kuzuia Rais John Magufuli asiwe Mwenyekiti wa chama hicho baadaye mwaka huu kama inavyotarajiwa na wengi, Raia Mwema limeambiwa.

Gazeti hili limeambiwa kwamba mkakati huo unapangwa kwa siri kubwa na kwamba utatekelezwa wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi ujao.

Vyanzo vya kuaminika vya gazeti hili vimeeleza kuwa kuna wajumbe ambao watasimama na kutoa hoja kwamba si lazima kwa Mwenyekiti wa CCM kuwa pia Rais kutokana na sababu mbalimbali.

“Kuna sababu kadhaa ambazo zitatumika. Kwa mfano, kuna watakaosema kwamba dunia nzima hivi sasa mfumo huo hautumiki. Nchi zinazotajwa kutotumia mfano huo ni Kenya, Afrika Kusini na hata Marekani.

“Hoja itakuja kwamba kazi za chama ni za chama na za serikali ni za serikali. Wataeleza kuwa Jacob Zuma (Rais wa Afrika Kusini) si Rais wa chama tawala (ANC). Rais wake anaitwa Baleka Mbeke.

“ Kuna wengine watatoa hoja kwamba katika hali ya sasa, kama Rais akichukiwa, basi na chama kitachukiwa pia kama mtu mmoja atashika nafasi hizo mbili.

Ni muhimu chama kiokoe serikali au serikali iokoe chama na si wote wazame kwa pamoja,” kilieleza chanzo hicho ambacho ni mmoja wa wanachama waandamizi wa CCM waliowahi kushika nyadhifa za juu serikalini.

Hata hivyo, mtoa habari wetu huyu ambaye aliomba kutotajwa jina kwa maelezo kuwa wahusika ni watu anaofahamiana nao vizuri; alisema kwamba ni wazi Rais Magufuli ana taarifa hizo na kwa vyovyote atajiandaa kupambana na hali hiyo.

Mmoja wa vigogo wanaotajwa kuhusika na mpango huu aliliambia gazeti hili kwenye mahojiano naye yaliyofanyika Dar es Salaam kuwa haoni kama ni tatizo kama kuna wana CCM wanaoamini kuwa utaratibu wa Mwenyekiti wa chama kuwa pia Rais wa nchi umepitwa na wakati.

“ Sikiliza, mimi sitaki unitaje jina kwenye gazeti lako kwa sababu ukifanya hivyo utakuwa tayari umenihukumu kwamba nimo kwenye huo mpango. Mimi sijui chochote.

“Hata hivyo, sidhani kama wanaofikiri tofauti wanakosea. Kama wataibua hoja hiyo, itapewa majibu na huo ndiyo utaratibu wetu ndani ya CCM.

“Kama watu wanaona kwamba kitu kimepitwa na wakati watasema tu. Tulikuwa na Azimio la Arusha baadaye likabadilishwa. Tulikuwa tumekataza wafanyabiashara kwenye siasa lakini baadaye tukawarudisha na sasa tunafikiria kuwatenganisha na siasa. Hayo yote ni mawazo”, alisema kigogo huyo ambaye ni mwanasiasa maarufu wa CCM ambaye aliwania urais na Magufuli katika mchakato wa ndani wa CCM mwaka jana.

Katika miaka ya 1990, aliyewahi kuwa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kuwaambia wanachama wa chama hicho kuwa ni muhimu kwa mtu mmoja kushika nyadhifa zote hizo kwa sababu ya umoja na utengamano ndani ya chama.

“ Mnaweza kuamua kuwa na Rais mtu mwingine na Mwenyekiti wa chama. Lakini omba Mungu wapatane maana wasipopatana itakuwa vurugu tupu,” Mwalimu alinukuliwa kusema wakati huo.
Katika historia ya CCM, ni Mwalimu pekee aliyepata bahati ya kuwa Mwenyekiti wa chama wakati Rais wa Tanzania akiwa Ali Hassan Mwinyi, lakini wanasiasa wakongwe kama Pius Msekwa wanaamini kuwa isingekuwa rahisi kwa Nyerere kuondoka ghafla madarakani kwa kuacha nyadhifa zake zote.

Katika mahojiano yake aliyowahi kufanya na gazeti hili nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Msekwa alisema kwamba anaamini Mwenyekiti wa sasa wa CCM, Jakaya Kikwete, atamuachia Magufuli wadhifa huo mapema.

“Katika historia ya Tanzania, ni Nyerere pekee ndiye aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM kwa muda mrefu huku mzee Mwinyi akiwa Rais. Lakini kulikuwa na sababu wakati huo kwamba Watanzania walikuwa wakimpenda sana Mwalimu na nchi ingetikisika kama angeachia nyadhifa zote mbili,” alisema Msekwa mapema mwaka huu.

Wakati gazeti hili likiwa na taarifa kwamba baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu huo tayari wameanza kutumiwa mialiko ya kwenda kuhudhuria mkutano huo, kuna wajumbe wameanza kudai kwamba mkutano huo ‘hautanoga’ kufanyika wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ulioanza wiki hii.

Raia Mwema limeambiwa kwamba sababu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mojawapo ya zile zinazoanza kuibuka sasa kutaka Mkutano Mkuu wa CCM usogezwe mbele, baada ya ile ya zamani ya ukosefu wa fedha kuonekana haina nguvu.

Gazeti hili limeambiwa kwamba baada ya viongozi wa CCM sasa kudai kwamba kuna matatizo ya kifedha, Magufuli mwenyewe ameamua kubeba mzigo wa kuhakikisha fedha zinapatikana kufanikisha hilo.

Mkutano huo unaweza kufanyika baada ya Bunge la Bajeti kumaliza mkutano wake mjini Dodoma mwishoni mwa mwezi huu ili kuwezesha wale watakaokuwa Dodoma kutohangaishwa kurejea makwao na kisha Dodoma tena kwenye mkutano huo.

Alipoulizwa na Raia Mwema kuhusu kama Magufuli amekubali kubeba mzigo wa kutafuta fedha za Mkutano Mkuu huo wa CCM na mambo mengine yanayohusu Uenyekiti wa CCM, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, alisema hana mamlaka ya kuzungumzia mambo ya chama.

“ Mambo ya CCM mimi yako nje ya uwezo wangu. Siwezi kukujibu ndugu yangu naomba tu uwaulize wenyewe kwa vile mimi niko serikalini na kwenye chama wana watu wao”, alisema.
Juhudi za kumpata Msemaji wa CCM, Christopher ole Sendeka, kuzungumza kuhusu suala hili hazikufanikiwa hadi tunakwenda mitamboni kwa vile ofisini kwake alielezwa kuwa yuko safarini kwenye mikoa ya Kusini na simu yake ilikuwa haipatikani.

My Take:

Vita ni kubwa sana ambayo raisi wetu Magufuli ameamua kuivalia njuga, na hata hili la mchungaji Gwajima ambae jana kutoa ujumbe wake kwa raisi Magufuli na "YULE", halijatoka bure.

Na hao wanachama wawili waandamizi wanaotajwa hapo kushiriki hii blackmail ni akina nani hao?

Raia Mwema nakuaminieni katika ubora wa taarifa zenu za uchunguzi.

Mzee Pius Msekwa na wazee wenzio kiokoeni chama hiki.

Watanzania tunakwenda wapi?
Tunakiobea kife kabisa naona kama kinachelewa kufa
 
Hawa waandishi wa habari nao wawe wanafanya home work zao kwanza!! Zuma ni Rais wa chama Baleka ni Mwenyekiti!!

Rais wa chama ANC ndiye mwenye nguvu zaidi. Ndiyo maana Mbeki alipooteza hiyo nafasi waliweza kum-recall na kupoteza cheo chake cha Ukuu wa nchi.

Nchi nyingi tu za kiafrika bado zinatumia huu mfumo wa CCM na Tanzania including Zambia, Uganda, Malawi, Rwanda, Namibia n.k.
Hizo zote ni mbwembwe hapa kikubwa ni kuiombea ccm ifie mbali
 
Tunakiobea kife kabisa naona kama kinachelewa kufa

Hahahahaaa, kufa hakiwezi ila kitapata msukosuko mkubwa.

Natamani tungepata wasaa wa kutazama mkutano mkuu "LIVE" kutoka Dodoma.
 
Ni vigumu sana kuibomoa ccm Jk akiwa bado ni mwenyekiti. Ila akikabidhi kijiti kwa Magu, Nina imani ccm no longer to stand as u see
Mkuu mwanzo wa hesabu ni moja na huu mtifuano ni moja ya hatua za kubomika kwa ccm
 
Naunga mkono hoja, asikabidhiwe nafasi zote mbili maana wananchi tumeanza kuingiwa na hofu na utawala huu
 
Tunasubiri mjumbe huyo ataesimama na hoja hiyo tuone! Manaa JPM ameshajua nani wako behind ya hiyo kitu ili kumpung nguvu na kumfanya asiguse interest zao! Inajulikana!! Ndio maana safari za Ikulu kwa mstaafu mmoja haziishi....akienda na mstaafu mwingine nae anaitwa!! Nadhani balance mkwara
Wacha hilo dubwana life kama alivyo liita gwajima
 
Hahahahaaa, kufa hakiwezi ila kitapata msukosuko mkubwa.

Natamani tungepata wasaa wa kutazama mkutano mkuu "LIVE" kutoka Dodoma.
Huo mkutano hautarajii kufanyika karibuni maana hata ela za kuendesha huo mkutano bado hawajapata
 
Back
Top Bottom