mohoziz joseph
Member
- Feb 26, 2013
- 30
- 47
RAI YANGU KWA KADA WA CCM NA MKUU WA WILAYA YA ARUSHA MJINI Mh Mrisho Gambo
Ndugu yangu, Kiongozi hodari Mrisho, naandika haya kwa nia njema kabisa kusaidia maendeleo ya Jiji la Arusha na watu wake.
Kabla sijaenda kwenye rai yenyewe naomba tujipitishe kwenye vipengele kadhaa vya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 Toleo la 2010.
Ibara ya 75 inahusu Vikao vya CCM Wilaya. Ibara ndogo ya 75(1) inaorodhesha Wajumbe wa Mktano Mkuu wa CCM Wilaya kuwa ni
a.
b.
c. Mkuu wa Wilaya ambaye anatokana na CCM
Ibara ya 96(2) inaeleza kuwa Mkutano Mkuu wa Wilaya ndicho Kikao Kikuu cha CCM Katika Wilaya.(unafanyika mara moja kwa mwaka ama mara nyingi itakavyohitajika)
Ibara ya 96(3) inaeleza kuwa Kamati ya Madiwani wa CCM itakuwa na jukumu la kusimamia kwa ujumla utekelezaji wa Ilani ya CCM katika shughuli zote zinazoendeshwa na Halmashauri.
Ibara ya 78(1)(c) inasema Halmashauri Kuu ya CCM itaundwa na wajumbe wafuatao
a.
b.
c. Mkuu wa Wilaya ambaye ametokana na CCM
Ibara ya 80(1)(c) inaeleza kuwa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya inaundwa na Wajumbe...
a.
b.
c. Mkuu wa Wilaya anayetokana na CCM
Ukisoma Ibara zote hizo zinamtambulisha DC kama Kada mwaminifu wa CCM. Mimi sina neno na ukada wa mtu na vyeo vingine vyote. Nina hoja na matumizi mabaya ya mamlaka na kuingilia mamlaka nyingine bila utaratibu hasa kwa kiongozi ambaye sio neutral, amebeba maslahi binafsi ya chama chake.
Nchi yetu imeanza kuingia kwenye mfumo wa viongozi kuacha kufuata sheria na taratibu na kujiendea wanavyotaka wao kwa maslahi mema au mabaya, kwa kujua au kutokujua. Waliobuni uwepo wa Sheria na Kanuni walikuwa na busara kubwa sana.
Leo hii madereva wa magari wanapokutana kwenye "round about" huoni wakigongana wala kukwepana kwasababu kuna mafunzo waliyapata kuhusu utaratibu wa kupishana maeneo hayo. Halikadhalika kwenye junction zenye taa za kuongozea madereva. Ni sharti uziheshimu, maana kinyume chake ni kusababisha ajali na maumivu au vifo.
Sasa ndugu yangu Gambo, wewe ndio umeanza safari ya maisha kama kiongozi kijana. Naamini unatamani kufika mbali. Nami nakuombea ufike mbali ilipo ndoto yako.
Niseme ukweli, kwa mwenendo ulioanza nao na papara za kufanya mambo kibinafsi kana kwamba Serikali haipo, utakucheleweshea kufikia ndoto kubwa.
Hakuna Kiongozi Mzuri duniani ambaye hafuati taratibu. Sisemi haya kuhofia utaisaidia CCM, hapana. Kama sio mwenyekiti wa CCM kuzuia mikutano ya kisiasa mngekuwa huru kujijenga. Kitu kibaya hapa ni vurugu na kuruvuga wananchi ilhali Serikali ni moja na wote mnaitumikia kwa niaba ya wananchi. Hilo ni baya.
Wewe na nduguzo Chadema ndio mnajijua mnatoka vyama tofauti na kila mmoja ana maslahi yake kisiasa. Lakini wananchi hawajui kama ninyi mnatoka Serikali tofauti. Wanajua Serikali ni moja na wanafahamu kuna Serikali Kuu na Serikali za Mitaa, ikiwemo hii Serikali ya Halmashauri ya Jiji.
Chadema na wananchi wanafahamu kuna Ilani kuu ya Taifa inayoongoza nchi, Ilani ya CCM. Wanafahamu pia kuna Ilani ya Chadema iliyoungwa mkono na UKAWA na ndio iliyowapa matumaini wananchi wakaacha kuichagua CCM wakaichagua CHADEMA
Wananchi hawa wanasubiri kutoa adhabu 2020 kama walilaghaiwa ama wameridhika na maamuzi waliyoyafanya. Wananchi wa Arusha ni waelewa sana. Wanajua kuhukumu. Wanajua haki na wajubu wao. Haikuwa bahati mbaya CCM kupata Diwani mmoja kati ya Kata 25.
Baraza la Hamshauri ya Jiji ambao ndio watunga sera na wasimamizi wa mipango ya Jiji lina wajumbe takribani 34; mmoja akitoka CCM na waliobaki wakiwa Chadema.
Kwa takwimu hizo inamaanisha kuwa CHADEMA wameaminiwa kwa miaka mitano hivi kutekeleza walichokiahidi.
Wananchi wa Arusha walishaachana na siasa za mifarakano na sasa wametulia wako busy na maendeleo. Kila mtu anapambana. Utulivu umerejea baada ya ghasia nyingi za makusudi na kukomoana miaka ya nyuma.
Nina ushauri mdogo, unaweza upokea ukiwa mwerevu au ukaupuuza.
Hakuna mtu anayekuzuia kwenda kuuliza shida za watu mitaani. Hauwezi kuzuiwa. Shida ni utaratibu unaoutumia unakuwa uko kisiasa badala ya kuwa kiserikali. Siasa mmezizuia na mwenyekiti wenu. Mngekuwa huru kufanya.
Sasa basi, wewe ni kada asiye na doa wa CCM. Kikawaida na kwa mujibu wa Katiba ya chama. Kama lengo ni kufanya siasa nakushauri kuzingatia maagizo ya Rais kabla hayabadilishwa na operesheni UKUTA au Mahakama kuwe FANYA MIKUTANO YA SIASA KWENYE MAENEO MLIYOSHINDA TU. Zunguka weee mpaka uchoke. Bahati mbaya Arusha Mjini CCM hamkushinda, Udiwani, Ubunge mpaka kura za Urais.
Kwa hapa Arusha Mjini waachie walioshinda wafanye kazi ya umma, usiwavuruge. Tangu wameshinda hawafanyi siasa. Wanafanya maendeleo kimya kimya. Usiingilie kati na kuwakoroga wananchi. Serikali ni moja, hakuna Serikali ya Mrisho na Halmashauri.
Jifunze kutenganisha majukumu ya uwakilishi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa. Zingatia majukumu halisi ya DC na mipaka yake.
Ukiwa lengo ni Kuharakisha Maendeleo na kutatua kero utapewa ushirikiano wote kama utaamua kuwa mshirika wa maendeleo na kushirikiana na viongozi wengine kama tulivyokuwa tukienjoy ushirikiano na DC Nkurlu na RC Ntibenda. Unaweza kuiga machache toka kwao na ukawa bora.
Chadema hawaongozi kwa kukurupukia mambo. Wanafuata sheria na taratibu. Wanatekeleza kwa mipango na vipaumbele (unless litokee jambo la dharura). Ni hatari kuwakoroga wananchi kwa suluhu mbili tofauti kwa jambo lilelile. Mbaya zaidi suluhu moja haina bajeti, haiko kwenye ratiba.
Haya matatizo unayoyatafuta leo yamekuwepo miaka zaidi ya 50 ya uongozi wa CCM. Chadema waliyapigia kelele pamoja na wananchi yatatuliwe yakapuuzwa mpaka walipoaminiwa wao kuyakabili wakiwa na mamlaka ya kuamua.
Matatizo hayamaliziki kwa kuzungukia Mitaa na kuyasikiliza. Matatizo mengine ni ya ngazi za huko mitaani usiposhirikisha wahusika utayahamidha na kuyafanya makubwa na huko watarelax ufanye juu.
Mh Gambo, wewe na Mh DED ni wageni kwenye Halmashauri hii inayoongozwa na Chadema. Mnapaswa kujipa muda kujua mini kimeamuliwa, nini kimefanyika , nini kipo kwenye utaratibu na ni gani ili ukienda huko mitaani na kutoa majibu yawe majibu ya Mamlaka ya Serikali na sio yako binafsi.
Kwa hiyo kama itakulazimu kuzungukia Nero bila kuitwa au kutaarifiwa, nenda Halmashauri wakupe mrejesho wa jambo husika kwanza. Tusiwakoroge wananchi. Naona unaenda unarudia mambo yaliyoamuliwa na kutoa majibu yanayopishana. Hii ni nini?
Sio lazima uambatane na Kiongozi wa Halmashauri. Muhimu ni ushiriikiano.
Kwa mfano, hali ya usalama na ulinzi wa wananchi na mali zao haujawa imara inavyotakiwa. Umeacha kushugulikia haya unaenda AUWSA kuomba maji ambayo utekelezaji unaendelea a Meya wa Jiji ni Mjumbe wa Bodi ya Maji. Ungeuliza kwanza kusingekuwa na marudio na kukoroga watu.
Ama la, ukiona nafasi ya ukurugenzi inakuvutia zaidi, turushusu tukuombee kwa Mh Rais akubadilishie nafasi, uwe DED nae awe DC.
Asante!