Kakke
JF-Expert Member
- Dec 4, 2010
- 1,883
- 1,482
RAHA YA KUWA NA MBUNGE WA CCM KATIKA JIMBO LAKO HII HAPA
"Mheshimiwa Spika, kabla sijaingia kuchangia bajeti hii, nataka niseme kuwa naona upinzani wamefikia pabaya sana, wanaikashifu serikali sikivu ya CCM. Chama kimefanya mengi sana, maendeleo makubwa tumepata, shule za msingi, sekondari na vyuo viko vingi sana tofauti na zamani, barabara za lami, umeme nchi nzima mpaka vijijini, lakini wapinzani wanakebehi.
Naipongeza sana serikali ya Chama Cha Mapinduzi. Mheshimiwa Spika, bila kupoteza muda sasa niingie kwenye jimbo langu, naomba nielezee kwa kifupi matatizo ya jimbo langu. Kule hatuna shule za sekondari katika kata sita, maji ni ndoto, tunategemea mvua za msimu. Shule zilizopo hazina ubora wala walimu wa kutosha. Rais alikuja sasa ni miaka sita akatuahidi umeme lakini mpaka leo hakuna lolote. Barabara ni mbovu hazipitiki.
Nauliza ni lini serikali hii (ya CCM) itatusikia na kutuletea maendeleo?"(Wab unge Makofi) kwa! Kwa! Kwa!. Naombeni sana tena sana jimbo langu liangaliwe kwa jicho la Huruma. Baada ya kusema hayo Mheshimiwa Spika, naunga mkono bajeti kwa 100%