Rage, Sophia Simba wapanda kizimbani

Lilombe

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
242
39
sofia%20simba.jpg
Sophia Simba



aden%20rage.jpg
Aden Rage

*Ni katika kesi ya uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga
*Rage aeleza bastola yake ilivyoonekana jukwaani
*Chakula alichokula Sophia Simba Igunga champonza
*Adai aliandaliwa na ndugu yake, ashindwa kumtaja jina

MBUNGE wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM), pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wamepanda kizimbani.
Rage na Sophia Simba walipanda kizimbani jana wilayani hapa ili kutoa ushahidi wa kesi ya kupinga matokeo yaliyompatia ushindi Mbunge wa Igunga, Dk. Peter Kafumu (CCM).

Kesi hiyo ya kupinga matokeo ilifunguliwa na mlalamikaji Joseph Kashindye dhidi ya Dk. Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Igunga. Kesi hiyo iliendelea kusikilizwa jana mjini hapa katika Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora.

Rage ambaye ni shahidi wa 15 kwa upande wa wajibu madai, alikiri kushiriki kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga, ambapo alipangiwa na chama chake kufanya uratibu katika Tarafa ya Igulubi wilayani Igunga.

Akiwa mahakamani hapo, Mbunge huyo wa Tabora Mjini, alitoa maelezo yake huku akiwa ameketi katika kiti kilichokuwa kizimbani hapo.

Baada ya kutoa maelezo hayo, wakili wa mlalamikaji, alianza kumuuliza maswali shahidi huyo juu ya umiliki wa bastola yake na kwa nini alikuwa nayo katika mikutano mbalimbali ya kampeni jimboni humo.

Wakati akijibu maswali hayo, Rage alikiri kumiliki bastola hiyo pamoja na kushiriki nayo katika shughuli nzima za kampeni wakati huo.

Hata hivyo, alisema upepo ulimponza hasa pale ulipopeperusha shati lake na kusababisha bastola yake kuonekana hadharani na kupigwa picha na waandishi wa habari waliokuwa mkutanoni hapo.

"Pamoja na kufanya mikutano mbalimbali hasa wakati nilipokuwa ninapanda kwenye jukwaa la kampeni, upepo mkali ulifunua shati langu na kusababisha bastola kuonekana hadharani na ndipo waandishi wa habari walianza kuniangalia na hatimaye walinipiga picha.

"Picha ile ilionekana katika Gazeti la Mwananchi la kesho yake,'' alisema Rage.

Alisema kuwa, baada ya kutokea tukio hilo, bastola hiyo ilichukuliwa na Jeshi la Polisi kwa maagizo ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kisha akahojiwa na jeshi hilo.

Alisema pia kwamba, pamoja na kuhojiwa pia alipigwa faini ya Sh 100,000 na Kamati ya Maadili ya Uchaguzi.

Katika utetezi wake huo, Rage alitumia zaidi ya saa tatu mfululizo, ambapo alisema suala la yeye kuwa na bastola lilimalizika baada ya Kamati ya Maadili kumpiga faini kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.

Wakati huo huo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, ambaye alikuwa shahidi wa 16 kwa upande wa mjibu madai, alitoa ushahidi wake ambapo alikiri kula chakula na wanachama wa CCM katika Hospitali ya Nkinga, Kata ya Inkiga.

Waziri Simba, alisema alishiriki kula chakula hicho baada ya kupata mwaliko kutoka kwa ndugu yake ambaye, yupo katika hospitali hiyo ingawa alipoulizwa jina la ndugu yake huyo alishindwa kulitaja.

Licha ya kula chakula hicho, Simba alisema alikula yeye pamoja na watu zaidi ya 50, hali ambayo iliwafanya mawakili wa mlalamikaji waendelee kumuuliza maswali, likiwemo la kudaiwa kuwahamasisha wasimchague Kashindye kwani hana mke na ni masikini, madai ambayo aliyakanusha vikali.

Kesi hiyo ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi Dk Kafumu, inasikilizwa na Jaji Mery Shangali na inaendelea leo.

Wakati ikiendelea, tayari mashahidi 22 upande wa mlalamikaji tayari wameshatoa ushahidi.

Source: Gazeti la Mtanzania, Mei 18, 2012
 
rage bishooo tuuuuu hana lolote. Hatuhitaji wabunge wa aina yake, sharobaro siyo sharobaro, basi tabu tu.
 
rage ismail///////kichefuchefu//////maji marefu,,lusinde,,,komba,,,,anna kilango,,,,,,,nk,nkbure kabisa:drama:
 
Back
Top Bottom