Rage aitabiria kiama Yanga

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Rage.jpg

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage
Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage ameitaka timu ya Mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga, wajiandae kupokea kichapo kitakatifu katika mechi ya Ngao ya Jamii itakayochezwa mnamo Agosti 23 mwaka huu katika uwanja wa Taifa.

Aden Rage amefunguka hayo ikiwa zimebaki siku chache kuanza kwa mtifuano huo huku akiwashangaa wanayanga kwa uwamuzi waliyoufanya kuenda kujificha mjini Pemba.

"Kama mimi ningekuwa kiongozi wa Yanga tarehe 23, ningesema hiyo Ngao ya Jamii wazee chukueni maana kila nikiangalia pale wa kumzuia Emmanuel Okwi, John Boko sioni, sasa Haruna Niyonzima naye zile majaro anazozitupa zinaleta raha, kwa hiyo nina uhakika tarehe Agosti 23, al manusura kama wamepata bahati watakula 7, sasa wanakuja kukutana na Simba. Sisi huko nyuma hatujapata ubingwa muda mrefu ni sawa sawa na Simba aliyejeruhiwa ukikukuta naye njiani hana msalie Mtume lazima akumalize tu. Na sijui wameenda Pemba kufanya nini, labda wanaenda tu kuchuma karafuu,” alisema Ismail Rage

Pamoja na hayo, timu ya Simba na Yanga zote kwa pamoja zimekimbilia mjini Zanzibar kwa lengo la kujiweka sawa kuelekea mtanange huo wa kukata na shoka ambao mpaka sasa kila mmoja anamtambia mwenzake kumfunga kutokana na ubora wa usajili waliyofanya katika msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania Bara 2017/2018.

Chanzo: EATV
 
Kwa kuzungumza tu Rage kajaliwa hicho kipaji...
Simba wapo vizuri sana kwenye eneo la uhabarishaji. wana hat trick ya magwiji kwenye eneo hili - Rage, Julio & Haji.

hopefully kuanzia msimu huu wataleta hat trick za mataji Msimbazi kama wenzao wa Jangwani wafanyavyo.

Yanga na nyinyi embu msimu huu legezeni kidogo - monopoly inaifanya ligi yetu iwe inaboa kama La Liga bana!!
 
Kwa hili naomba Julio umtoe. Ameshasema kwamba Simba wasihadaike na ukimya wa Yanga, bado ina moto. Isipokuwa kama alisema hivyo kununua kura za wajumbe wa Yanga kwenye uchaguzi uliomalizika (naye akamalizika) wa TFF.
 
View attachment 566964
Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage
Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage ameitaka timu ya Mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga, wajiandae kupokea kichapo kitakatifu katika mechi ya Ngao ya Jamii itakayochezwa mnamo Agosti 23 mwaka huu katika uwanja wa Taifa.

Aden Rage amefunguka hayo ikiwa zimebaki siku chache kuanza kwa mtifuano huo huku akiwashangaa wanayanga kwa uwamuzi waliyoufanya kuenda kujificha mjini Pemba.

"Kama mimi ningekuwa kiongozi wa Yanga tarehe 23, ningesema hiyo Ngao ya Jamii wazee chukueni maana kila nikiangalia pale wa kumzuia Emmanuel Okwi, John Boko sioni, sasa Haruna Niyonzima naye zile majaro anazozitupa zinaleta raha, kwa hiyo nina uhakika tarehe Agosti 23, al manusura kama wamepata bahati watakula 7, sasa wanakuja kukutana na Simba. Sisi huko nyuma hatujapata ubingwa muda mrefu ni sawa sawa na Simba aliyejeruhiwa ukikukuta naye njiani hana msalie Mtume lazima akumalize tu. Na sijui wameenda Pemba kufanya nini, labda wanaenda tu kuchuma karafuu,” alisema Ismail Rage

Pamoja na hayo, timu ya Simba na Yanga zote kwa pamoja zimekimbilia mjini Zanzibar kwa lengo la kujiweka sawa kuelekea mtanange huo wa kukata na shoka ambao mpaka sasa kila mmoja anamtambia mwenzake kumfunga kutokana na ubora wa usajili waliyofanya katika msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania Bara 2017/2018.

Chanzo: EATV
Maalim Ustaadh Ismael Aden Rage si mtabiri wa kuaminika. Alishindwa kujitabiria kifungo alipokuwa Katibu Mkuu wa FAT. Utabiri wake ulipomwambia Mbuyu Twite angetambulishwa kwenye Simba Day kama mchezaji wa Simba, akaishia kwenda Yanga. Kabla ya hapo alishakosea kwenye utabiri wake kwamba Yondan ana mkataba na Simba, naye akaishia Yanga. Kwa hivyo kwenye mpira, hasa kuhusiana na vita ya Simba na Yanga, utabiri wake ni wa kinyumenyume. Huenda basi tafsiri ya utabiri wake huu ni kinyume cha aliyoyasema pia. Nje ya soka, akashindwa kujitabiria kushindwa kutetea kiti chake cha Ubunge Tabora Mjini. Mwanzisha uzi tuletee utabiri mwengine wa mtu anayeaminika zaidi kwenye hii fani. Hatutaki utabiri wa 'labda' kama huu.
 
Kusema mtakula 7 ni kosa la Jinai?

Basi tufanye 8 mkuu kama unaona hazitoshi
Kwa wachezaji gani?wamekuja kuchukua pension Simba...hapo Simba hakuna mchezaji atakayefunga double digits..labda kichuya penalts
 
Nae kama yule white tu.. Huyu c ndo kawajaza upepo wenzake waende FIFA wakate rufaa akiwaaminisha watapata point 3,...Sasa tumuulize, hiyo Thimba tarehe 23 inakuja kucheza kama nani? Na huyu ndo aliwaita wenzake mambumbumbu kwakua akiwaletea Okwi, basi wanasahau yote, ikawa anajipigia hela tu, turufu yake Okwi... Hahahaaah..

"Ukifuga njiwa utajua bei ya mtama"
 
Wahenga wa zamani walisema mtu akitoka jela ni lazima afanyiwe tambiko kuondoa ukichaa alioukwaa akiwa huko vinginevyo atakuwa kichaa siku zote.

Rage anastahili kuwa Mirembe! Ni mtu gani mwenye akili timamu atakwenda kwenye jukwaa la siasa pasipo na ghasia yeyote akiwa amejifunga bastola kiunoni mwake? Kama hilo linawezekana kwake atashindwaje kupayuko hovyo?
Rage.png
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom