Rafiki Yangu...

Mentor

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Posts
20,334
Reaction score
23,940
Rafiki yangu…

Wakati nikiendelea kutafakari mustakabali wa mdogo wangu wa mwisho ambaye tayari ameshakwenda Form five na kusahau machungu ya matokeo yao halafu wanaambiwa mitihani imefutwa itasahihishwa tena.

Nilijua si wote waliofeli ni kwa sababu ya maisha ya siku hizi ya watoto kuwa facebook muda wa vipindi kwani yeye namfahamu sana. Anapenda kusoma sana ila matokeo yale hayakuwa sahihi….anyway, hilo si la leo bado nalitafakari.

Katika tafakuri zangu nikajikuta nimefika MUHAS...famously known as MUHIMBILI. Hapo napo kuna mdogo wangu ( Asnam) yuko mwaka wa nne pale akisoma shahada yake ya kwanza ya udaktari.

Basi tukatoka for lunch and while there ndipo aliponielezea story ya rafiki yangu KakaKiiza..hata sijui kama bado nastahili kumuita rafiki.


[B KakaKiiza na Mentor
[/B]

Mimi na KakaKiiza tumetoka mbali. Kwanza tulikuwa majirani hivyo michezo ya utotoni tuliicheza pamoja. Tumesoma wote tangu O’level kule Agape Lutheran Junior Seminary..tukarudia wote mitihani ile ya 1998. Nakumbuka walikuwa wakiniita MCHUNGAJI. We were still friends mpaka A’level tukaenda wote Moshi Sec. We were still buddies tukapangiwa wote chuo yeye akaenda UDSM kusoma BCOM mimi Ardhi University kusoma Architecture. He used to come home na akawa anafahamika. Wadogo zangu wote walikuwa wanamheshimu na kumpenda kama kaka.
Baada ya hapo mi nkaenda zangu Dodoma kufanya kazi nayeye akarudi Moshi kuendelea na biashara za wazazi wake.

September 2010

Mwaka huu KakaKiiza alijiunga na Masters program tena palepale UDSM. So kama family friend nkamwambia afadhali upo Dar kuna mdogo wangu yupo Muhimbili utakuwa unamcheki na yeye ajisikie kama ana kaka. Akakubali.

So nikampa namba za simu za mdogo wangu…woe unto me!!!!


Fast forward to Friday, 2[SUP]nd[/SUP] May 2013

Nimekuja Dar kufuatilia kitabu changu ninachoandika na kukifanyia printing pale UDSM Printing Press. So nikampigia mdogo wangu simu kama yupo free. Akaniambia ndo ametoka cadaver practical na hana tenda kipindi. Nikamwambia nampitia anisindikize UDSM.
Safari yetu baada ya kumaliza kufuatilia kitabu na logistics zingine ikatufikisha Brajec kula. Ni hapo ndipo aliponipa stori ya KakaKiiza, my friend.

Ilianza kwa kumpigia simu usiku na kumtumia vocha. Asnam akaona ni jambo la kawaida..si ni kaka kanitumia? Siku nyingine anakuja kumsalimia Muhimbili pale anamuuliza kama ameshakula au bado. Mara nyingi alikuwa akimwambia ameshakula hasa kwa sababu ya ratiba ngumu ya shule asingeweza kutoka. Maana kila weekend KakaKiiza alikuwa anakuja kumsalimia..what a brother!!!!!!!!!

Siku moja weekend kama kawa KakaKiiza akaja kumsalimia halafu akamuuliza kama ameshakula nay eye akasema bado. Akamwambia twende tukale. Akaingia kwenye gari haooooo…kushtukia yuko Sinza…bar si bar…Kelele..pombe nyingi…hakuna chakula kuna nyama tu..ikabidi waagize tu nyama. Eventhough dogo anasema alikuwa na njaa kweli.

Shida ikaja kwenye drinks. KakaKiiza akaagiza Safari zake na mdogo wangu akaagiza Sprite. Mhh..akaanza kumlazimisha anywe hata amarula sijui na nini. Hapo ndo dogo akashtukia ameingia mkenge leo. Lakini huyu si ni kaka yetu jamani? Mbona anageuka tena? Mara hataki kukaa mbali nay eye so akasogeza kiti karibu yake. Mara aweke mkono wake begani mwake..aah alimradi shida tupu. Muda unazidi kukatika.. KakaKiiza anazidi kulewa..nyama haziji..kelele…njaa na usumbufu wa kakakiiza.

Ngoja nijiweke kwenye viatu vyake kwanza niendelee kuhadithia…kuanzia sasa Asnam (mdogo wangu) ndo anahadithia…

Alikuwa na ki-pimple chini ya kidevu halafu kwanza alikuwa ameshakipasua. Akaniambia nikipasue. Nikamwambia angoje kiive tena ndo akipasue akikipasua tena kitakuwa kidonda. Mara ananing’ang’aniza nikipasue. Akamwita na waiter amletee tissue. WTH..nikamwambia … KakaKiiza unapoteza muda wako tu siwezi kufanya kitu kama hicho.

Nikaona hapa ameshaanza kulewa hatutaelewana. Nikamwambia anirudishe chuo. Na nikamwambia, “ KakaKiiza, Next time you want to take me out, don’t bring me to such places. I hate noisy places and I prefer real food” Akasema, “I know the right place.” Tukaondoka ikabidi nibebe nyama zangu bila kuzila.

Kwa sababu ya giza lile sikujua tunaenda wapi ila nkashtuka tupo outside Makumbusho. Nilikasiirika sana yani nikamwambia nataka kwenda chuo sio hapa. Eti akashuka kwenye gari akaenda kula minyama yake nje. Mi nkabaki ndani namuangalia tu anavyokula vibaya kama nguruwe. Kwanza hajanawa..anashika nyama na limkono lote..yani alinkera sana ile siku.
Akaingia ndani ya gari na mamikono yake michafu anaendesha huku anataka kunishika mkono..yuuuuuuck!!! yani ikabidi nijifanye kila saa niko kwenye simu tena nimeishika na mikono yote ili tu asinshike.

Akanirudisha chuo..nikashuka haraka sana tena wala hata sikumuambia asante wala nini. Nilimshusha hadhi sana ile siku. Nakumbuka neno lake la mwisho ile siku lilikuwa, “Dogo nimeupenda msimamo wako” Na tangu ile siku hajawahi kunipigia wala nini.
Ndo marafiki zako hao….


Wasalaam wapendwa,
Mentor.

 
Last edited by a moderator:
Hivi mwanaume akimpenda dada wa rafiki yake ni dhambi??

Kupenda si tatizo..ila kwa hili haikuwa kupenda aisee! mtu ukimpenda utamheshimu..!

Lingine ni age difference mimi na KakaKiiza, Kipaji Halisi, shem sosoliso, na Arushaone tunaelekea umri mmoja 35 na mdogo wangu ni ka-sweet sixteen ka 23yrs...!!! SITAKI URAFIKI TENA>..:mmph:
 
Last edited by a moderator:
Mentor ulikuwa wapi maana ni siku nyingi sana haujaonekana humu ndani karibu tena
 
No offensive, its just a wrong move at a wrong time....if he was carefull and gentle enough....you won't even know.Ila kwa hqpa ubaya ni kuwa namba ulimpa wewe pia amejaribu kutumia advantage.Pole lakini usimchukie mwambie dogo kanihadithia mlivyokosa chakula sinza....anaendelea kuwa rafiki japo mnatofautian kwa hilo.
 

Kwani kama mdogo wako Asnam angempenda KakaKiiza wewe ungempinga kisa ya age difference zao?

BTW Mentor usilalamike bhana maana kama KakaKiiza asingefanya hivyo ungesema "oooh KakaKiiiza hana lolote, yaani nimemkabidhi mdogo wangu ila mpaka sasa hajaonesha dalili yoyote ya kutaka kuunganisha undugu wetu".

Mara utakuja na manno ya kumponda Kiiza huku ukisema "sijui Kiiza sio rijali? maana sioni mchakato wowote ambao anaufanya kuhusiana na mdogo wangu?"
 
Last edited by a moderator:
Mentor ulikuwa wapi maana ni siku nyingi sana haujaonekana humu ndani karibu tena

Nipo ndugu yangu majukumu tu ya kulijenga taifa yaliongezeka kipindi fulani. Halafu nilimsindikiza kaka Mtambuzi msibani.



Very wrong move...wrong time..wrong person. Huyu ni mtu aliyemheshimu kama kaka tangu wakiwa wadogo.
So amechukua advantage ya ile trust kwake akaifanya mtaji wa kumtongozea mdogo wangu.
HAHh...eti nimwambieje!??



Hapo metaka kuuvunja undugu. Maana angefanikiwa hakika nisingalimsamehe.


Hahahaah saudari, really!?? Unamfahamu kakakiiza vizuri lakini? Muulize Vin Diesel na babu Asprin wakupe sifa zake.

Ila pia ndo kumpeleka mdogo wako Sinza kweli eti ndo mkale chakula? chakula gani na ofa za Redds sijui Savana eti pombe za wanawake...pambafff zake!!!
 
Last edited by a moderator:
Mentor swali la kichokozi huyo KakaKiiza hadi muda huu bado anasaka tuu hajaweka jiko ndani au alitaka amfanye Asnam jiko la pembeni aise

Asavali umeuliza. Mimi alishawahi kuntambulisha kwa amu kuwa ndo mchumba wake. Siku nyingine nkamkuta na Madame B, in short, tabia yake siielewi elewi!!!
 
Last edited by a moderator:
hii kali. Ila wajameni twendeni mbele na kurudi nyuma zamani dada wa rafiki yako alikuwa dadako kweli na ulimtreat kama dada au mdogo wako. Hisia za mapenzi ilikuwa ni ngumu sana kuziamsha bila kuwa na uhakika kuwa unachukua jumla. Siku hizi ninaona kama si sahihi unless uwe na uhakika kabisa kuwa huyu ndiye ama sivyo ukichukua na kuacha unauhatarisha urafiki wako na mwenzio unless ulikuwa urafiki mbuzi.... kitu ambacho sio rahisi kwa wanaume.
 

Wewe umenielewa na kama ni darasani nakupa 105%.

Kwa hili nahisi ni Kiranga peke yake atakayebisha!
 
Last edited by a moderator:
Huyu atakuwa mzabzab tu, bora umpe pesa zitafika ila ukimpa dada au mkeo amsindikize lazima majanga njiai . Sijakuona muda jamvini...upo?
 
Last edited by a moderator:
wadada wa chuo mnapenda vya bure sana wacha mliwe 2.na hapo ume2ficha 2 c mlimalizana kwenye gari humohumo.
 
Wewe umenielewa na kama ni darasani nakupa 105%.

Kwa hili nahisi ni Kiranga peke yake atakayebisha!

Mie nitambishia kidogo MwanajamiiOne. Naona kama ameangalia issue kwenye side moja ya coin tuu.

Nafikiri hii practice ipo prevalent zaidi kwa akina dada hasa kama kaka zao ni wastaarabu.

Nina maana wewe Mentor unanitambulisha kwa dada yako tena kwa wema kabisa.

Kwa kuwa anaku-regard as the best brother ever, basi ana-assume kuwa na mie rafiki yako nitakuwa kwenye category hiyo hiyo.

Mie nam-treat kama dada yangu lakini yeye yeye anakuja mazima mazima kwa kuona kuwa this is the golden chance to be missed.

Tena anafanya siri bila hata wewe Mentor kujua. At the end of the day unakuja kuambiwa tarehe ya ndoa.

How would you feel? Horrible? Proud? Mixed feeling?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…