Habari zenu humu ndani... mi mwenzenu ninatoka Na mme wa mtu ndo mbaba WANGU Na ananiweka mjini mwaka sasa.. kuna kipindi cha nyuma tulienda zetu huko sehem ya mbali kidogo kubadilisha hali ya hewa. Sasa akanitambulisha kwa rafiki zake ambao walikua wakifanya kazi pamoja ila baadae wakatenganishwa.
Kijana mmoja akaonesha kama kanizimia mana alivokuja akanisalimia akanishika mkono kama shemeji ake .
Sasa tukakutana gafla siku nyingine tukapeana namba. Sasa kijana akanipenda tangu ile siku kiukwel nilipomuona pia nilijikuta navutiwa nae. Basi tumewasiliana Na nampenda Na tumepanga mikakati mingi Na soon tunataka tukatambulishane ili mwakani mungu akipenda tuoane.. MTIHANI UNAKUJA HAPA. mchepuko ananipenda mpaka basi Na hii ni kutokana tunaheshimiana Na naiheshimu familia yake.Je naanzaje kumwambia huyu mtu??? Na mi najua hatoweza nioa kwa mara ya pili,Na mi kijana tumeelewana vema.
Ebu wenye upeo wanipe mawazo Na ushauri jinsi ya kumwambia huyu baba pia nahitaji maneno ya busara maana asije akafa kwa presha.
Wale mliozoea kutukana sihitaji comments zenu Za matusi... muwe wastaarabu kwani hakuna asiejua kwamba kuna kuchepuka au kutembea Na mke au mme wa mtu.. huwezi kushauri pita tuu kwa ustaarabu.
Karibuni kwa msaada