Rafiki Niliye Nae

Rafiki Niliye Nae

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
1,080
Reaction score
1,448
Dhiki

1 Naomba kuwauliza, majibu yawe mezani
Hayano ndoyaniliza, sijui nimekosani
Yataka kunimaliza, mwenzenu nitaabani
Rafiki niliyenae, katu ataki niwata

2 Amenigomea hasa, hunitoka na kurudi
Ngozi yake kama kasa, aniumiza fuadi
Nataka kufanya masa, nione lake kusudi
Rafiki niliyenae, katu ataki niwata

3 Namsema asikie, tena kwa jina mujue
Huko mkasimulie, na nataka nimuue
Dhiki 'sinishikilie, angalau nipumue
Rafiki niliyenae, jina lake ndilo dhiki

[emoji2399]Abuuabdillah[emoji3578]
Omari Juma Kimweri
0744883353
 
Back
Top Bottom