Rafiki "mwenda zake"

Rafiki "mwenda zake"

Bodhichitta

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2015
Posts
446
Reaction score
976
Habari members

Nimetumia neno mwenda zake kumaanisha amefariki.

Akili Leo imenikumbusha juu ya huyu rafiki yangu ambae ametangulia mbele ya haki akiwa mdogo saana miaka 32, ni huzuni sana lakina haikuwa na namna.

Kilichonifanya nimkumbuke na kuandika hapa huyu jamaa kwangu ilikuwa kama ni malaika muonyesha njia, nikiwa na maana kwamba kwangu alikuwa malaika ambae alikuwa ananionyesha sehem za mafanikio.

Yaani ni kama vile mungu alimleta Duniani kwa ajili yangu, nilistushwa saana na taarifa za kifo chake.

Iko hivi huyu rafiki nilikutana nae o-level japo huko hatukuwa karibu saana maana tulikuwa tunagombania nafasi darasani, yeye nafasi yakwanza mi yapili kwahiyo nilikuwa namvizia azubae tu niikanyage nafasi yake so Hilo likatufanya tuwe mbali.

Baada yakumaliza o-level tulipangiwa shule tofauti za advance Hilo likatufanya tupotezane.

Kama unavyojua hizi shule zetu za kata mara nyingi zinachukua wanafunzi wa vijiji jiran tu hili likatufanya tukutane baada yakumaliza advance.

Bahati ilioje tukapangia chuo kimoja japo campus tofauti then huko ukaribu wetu uliongezeka tukawa tunashirikiana na kusaidiana kwenye mambo kadhaa, mpaka tunamaliza then tukaja mtaani jamaa akabaki dar mi nikaamua kurudi home kwetu kijijini.

Nimekaa kwa mara ya kwanza jamaa akanitumia tangazo lakazi akaniambia omba kaka ujaribu zari nikaomba nikapata ilikuwa nikazi ya muda tu.

Nikarudi kitaa baada ya kumaliza haikuchelewa jamaa kunitumia tangazo lingine nikaomba nikapata, kwenye hii kazi yapili ilinishangaza kidog maana miongoni mwa tuliopata Mimi tu ndo ambae nilikuwa Sina ndugu mle ofisin wenzangu wote walikuwa na ndugu mpaka wenyew wakawa wanajiuliza imekuaje,
Nayo hii ilikuwa ni ya mda baada yakumaliza nikarudi kitaa kama kawaida.

Nilikata home kama mwaka hivi mwamba akanitumia Tena tangazo omba Hilo mwanetu nikaomba ila kwenye interview ya practical nikafanya vibaya mno nikajua pale nimefeli, majibu yanatoka nimepata.

Nahii nayo ilikuwa nikazi ya mda nikaenda nikafanya nikamaliza.

Yamwisho ndo hii ilikuwa mwaka 2019 mwamba akaniunganisha na mtu nmcheki Kuna watu wanatakiwa kama utafiti basi utachukuliwa nikamwambia poa, kaniunganisha nae kumcheki Ngoma ikatiki nikaenda kufanyakazi kule kwa miaka miwili baada yakumaliza pale Kuna mteja kwenye Ile ofisi niliyekuwa nafanyia kaz kanichukua na mpaka sasahiv Niko kwa huyo boss napiga kazi.

Sasa mwaka Jana mwezi wa 4 akanipigia simu kuniomba nimfanyia application za tamisem yeye Hana simu ameuza mambo yalikuwa magum, nikamwambia sawa kaka nikamfanyia application tukaomba dua fresh tunasubiri.

Tarehe 25 mwezi huohuo wa 4 napewa taarifa kuwa jamaa amefariki.. dah akili iliganda nilikumbuka mengiii
Nikaja kukumbuka kuwa jamaa kaenda sijamlipa fadhila zake na wala sijawahi mwambia kuhusu hili.
Duh ndo imekuwa basi Tena ametimiza mwaka mmoja sasa hivi.

Huyu naamini ndo alikuwa malaika wangu mwonyesha njia, mungu amrehemu kwakweliii

Kama nawe unae rafiki au ndugu wa namna hii tafadhali tushirikishe kwako mwonyesha njia kwa namna Gani lakini pia mpe maua yake anuse akiwa hai.
 
🥹🥹
 
Tafuta tumbo lililomleta duniani utoe sadaka, natumai msibani ulikwenda hivyo uliwaona wazazi wake. Wape hao fadhila. Waeleze pia ni jinsi gani mtoto wao alikuwa mtu muhimu kwenye maisha yako.
Usiingie roho ya choyo kwenye hili jambo.
Lakini na wewe kwanini mwenzio hana simu si mngeenda dukani umnunilie? ( kipindi hiko hukujua kama "ataenda").
 
Back
Top Bottom