Nilichojifunza ukiolewa ukamkuta mume ana rafiki yake ambae ameoa usijitie kimbelembele cha kuwa na urafiki na mke wa shemeji yake mara nyingi urafiki huo huwa hauwork out ni unafiki.
Nina case 3.
1.Recently kuna wadada wawili malkia wanguvu marafiki zangu waume zao marafiki basi huyu anapiga simu kwa wengine kumponda mwenzake na mwingine naye anahangaika kumponda mke wa shemeji yake.
Siku yao moja nitawaamulia nitawarekodi nitawafungulia group nitatuma voice notes zao wakisemana kisha naleft wapambane wajinga sana hao kuoneana wivu wa kijinga.
2.Case ya pili hubby alitakaga niwe na urafiki na mchepuko wa rafiki yake.
Yaani eti huyo rafiki yake ameoa mkewe yuko masomoni sasa ana kamchepuko kanajitegemea, wanaume walikuwa wana project yao tukajikuta na sie tunashiriki.
Mhhhh si unajua ile ego tena mke wa ndoa nitaundaje urafiki na mchepuko nikawa bandidu balaa kadada kanajidai kanajitahidi kujenga urafiki mimi nakaza uso.
Eti kuna siku tunaenda kula sikukuu ukweni hubby anapropose tuende nae. Nikamuambia wee vipi mke wa jamaa akirudi tena awe rafiki yangu? Nikalianzisha au hako kadada kamekutafutia mchepuko ndo maana unakapenda? Nililianzisha balaa.
Kuna siku wameenda kwenye mishe na le hubby mie nilikuwa naumwa hakyaMungu wamerudi nikawanunia na sikumtengea chakula hubby yule dada alipataga tabu na mimi sana. Kiufupi haikuwork out.
3.Mke wa rafiki wa mume wangu huyu wa ndoa kabisa nilimpenda balaa nikawa nikinunua kitu namnunulia malavidavi kama yote. Na yeye anashow love. Siku niliyosikia akiongea na simu kuwa najishaua na kujidai.
He he he he he nikachange na kila kitu kikaishia hapo kila mtu akala kona.
My dia wewe komaa na mume wako huyo ana sababu zake asikupasue kichwa.
Ukute mume wake anamchepuko huko basi anahisi labda mume wako anaujua au wewe unajua au kichaa cha ndoa kimempanda.