Rafiki kununa bila sababu

sweetdada

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2011
Posts
519
Reaction score
170
Wadau natumai mu wazima.

Naombeni ushauri. Nimetokea kuwa na urafiki na.mke wa rafiki wa mume wangu kwa muda sasa. Tumekuwa tukiwasiliana tukionana tukitoka out. Bahati mbaya ana changamoto kwenye ndoa yake so muda mwingi natumia kumliwaza na kumshauri.
Cha kushangaza amekata mawasiliano tangu juzi alhamis alinitumia ujumbe kunialika kwa pasaka nikamjibu nitaconfirm na mr kisha nimerudia. Tangu hiyo siku hapokei simu zangu na wala hajibu ujumbe. Nimemuuliza kama nimemkwaza kitu napo hajibu. Je nimpotezee au nimtafute ili nijue tatizo ni nini?
 
Mtafute umuulize tatizo ni nini if that friendship means so much to you.! If it ain't then kila mmoja ashinde match zake.! Wakati mwingine siyo lazima uwe na urafiki na kila mtu..!!
 


muulize Mumeo dear he gat nice advice to you babe.
 


labda anakutaka maana after mention your husband to him, he refuse to respond .. mi ningekuwa wewe ningempotezea because .. life is too short💣 mtu hata kiwi Kukutreat bad
 
labda anakutaka maana after mention your husband to him, he refuse to respond .. mi ningekuwa wewe ningempotezea because .. life is too short💣 mtu hata kiwi Kukutreat
Ni mwanamke huyu
 
Muulize kwa Upole na unyenyekevu rafiki yako. Ikiwezekana muonane live.

Ukimaliza huko, muulize mumeo kwa umakini pia.

Hope utapata jibu zuri tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
'Mke wa rafiki wa mume wangu'???

Sijaelewa apo kiongozi.nieleweshe nielewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ishi maisha yako tafuta vitabu soma hata magazeti yapo soma,fanya vitu vyako muda mwengine mnajitia stress kwa mavitu ya watu bure atajirudi mwenyewe tu kama hakujibu na hakuna kosa,hataki kusema kosa!
We jiulize kwanini unaishi..?? Kama msingi wa kuishi kwako ni hayo basi poteza muda wako huko lkn Kama si hapo yanini kujisumbua na mtu asiejisumbua nawe...!!!
 
Nilichojifunza ukiolewa ukamkuta mume ana rafiki yake ambae ameoa usijitie kimbelembele cha kuwa na urafiki na mke wa shemeji yake mara nyingi urafiki huo huwa hauwork out ni unafiki.
Nina case 3.
1.Recently kuna wadada wawili malkia wanguvu marafiki zangu waume zao marafiki basi huyu anapiga simu kwa wengine kumponda mwenzake na mwingine naye anahangaika kumponda mke wa shemeji yake.
Siku yao moja nitawaamulia nitawarekodi nitawafungulia group nitatuma voice notes zao wakisemana kisha naleft wapambane wajinga sana hao kuoneana wivu wa kijinga.

2.Case ya pili hubby alitakaga niwe na urafiki na mchepuko wa rafiki yake.
Yaani eti huyo rafiki yake ameoa mkewe yuko masomoni sasa ana kamchepuko kanajitegemea, wanaume walikuwa wana project yao tukajikuta na sie tunashiriki.
Mhhhh si unajua ile ego tena mke wa ndoa nitaundaje urafiki na mchepuko nikawa bandidu balaa kadada kanajidai kanajitahidi kujenga urafiki mimi nakaza uso.
Eti kuna siku tunaenda kula sikukuu ukweni hubby anapropose tuende nae. Nikamuambia wee vipi mke wa jamaa akirudi tena awe rafiki yangu? Nikalianzisha au hako kadada kamekutafutia mchepuko ndo maana unakapenda? Nililianzisha balaa.
Kuna siku wameenda kwenye mishe na le hubby mie nilikuwa naumwa hakyaMungu wamerudi nikawanunia na sikumtengea chakula hubby yule dada alipataga tabu na mimi sana. Kiufupi haikuwork out.

3.Mke wa rafiki wa mume wangu huyu wa ndoa kabisa nilimpenda balaa nikawa nikinunua kitu namnunulia malavidavi kama yote. Na yeye anashow love. Siku niliyosikia akiongea na simu kuwa najishaua na kujidai.
He he he he he nikachange na kila kitu kikaishia hapo kila mtu akala kona.

My dia wewe komaa na mume wako huyo ana sababu zake asikupasue kichwa.
Ukute mume wake anamchepuko huko basi anahisi labda mume wako anaujua au wewe unajua au kichaa cha ndoa kimempanda.
 
Matatizo tuu na ww usimsusie ataziidi kuwa na hali mbaya
 
Kuna kitu kasikia, acha kujipendekeza kwa mme wake.
 
Ngoja kwanza tudadafue.....hii sentensi (Mke wa rafiki wa mume wangu)... Hapa inamaana mume wako ana rafiki yake wa kiume ambaye ameoa kwahiyo mke wake una urafiki naye so nyie ni kama mtu na wifi yake....Sasa kama wifi amekununia unapata stress gani wakati mtu mwenyewe hata kwenye ukoo hayupo....watu hatuongei kabisa na ndugu wa damu sembuse huyo hata undugu hamna halafu unaumiza kichwa mpaka unakuja JF kutafuta ushahuri....hebu mpotezee maaana hakupunguzii wala kukuongezea kitu....au labda anakutaka mkasagane..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akii mi ningekausha kimya siku akijiskia kunambia atasema, mambo ya kubembelezana nop unless kuna kitu unajua umeharibu either umemuongelea Uongo labda. Ila kama sivyo subiri atakutafuta mwenyewe.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…